Wana janvi nimeleta mada hii baada ya kufikiri kwa miuda mrefu madhara yanayotokana na kelele lakini watanzania tunaonekana kutojali hata kidogo. Nimekuwa nilitembelea jiji la Dar es salaam nikapata shida sana, jirani ya hotel nilikokaa kulikuwa na mziki mkubwa, nilipouliza wenye hotel kuna nini jirani wakaniambia eti ni sherehe ya mtoto mchanga ya kufikisha siku arobaini !! Mziki ulipigwa usiku kucha nikaanza kujiuliza je huyu mtoto wa siku arobaini si wanamuua masikio? Sijafanya utafiti lakini ninahisi kuna watoto wengi watakaokuwa mazezeta kwa ujinga kama huu.
Nilipofika maeneo ya vijana nikakuta mziki unapigwa mango garden usiku kucha nikajiuliza watoto wanaoishi maeneo hayo wanafanya homework kweli? bila shaka watoto wanaoishi maeneo haya kitu homework hawakijui na uwezo wao wa kuperform shuleni lazima utakuwa wa chini tu.
Hapa jijini Arusha mji unakuwa kama hauna mwenyewe, unaweza kuwa uko ofisini asubuhi unaanza kazi ukasikia mziki mkubwa unapigwa na magari barabarani eti wanafanya matangazo, kwa kufanya hivyo wanafanya ufanisi wa kazi unashuka maana inabidi usubiri wapite ndo uendelee na kazi.
Kwa ujinga kama huu uchumi wa nchi unaweza ukawa unashuka bila kujua kumbe kuna sababu nyingine kama hizi ambazo viongozi wasioweza kufikiri kwa undani hawawezi kung'amua.
Naomba tujadili kama kuna sheria inayoweza kutusaidia ili tuwasaidie watoto wetu na sisi wenyewe, Kagame alishaagiza makanisa na misikiti kutoweka vipaza sauti maana mida ya ibada wanaifahamu.
Nawakilisha