Hivi tunakosa basic decency kabisa jamani?

Pundit,

Ukosefu wa maadili miongoni mwa jamii yetu unachangiwa sana na uovu huu mbaya unoendelea sasa. Science na teke linalokujia ndiyo ame acceralate uovu huu. Watu wanshindwa kuitumia hii fulsa ya kuwa na Mtandao na kuanza kuitumia kwa nia isiyokusudiwa kabisa. Lakini haya tufanyeje maana mtu huyu anayefanya haya ni jibaba au jimama lizima kabisa na heshima zake nyingi tena linaaminiwa mpaka linafanya kazi nyeti za benki. WanaJF yafaa kujua kuwa Ibilisi anatumia watu bila kujali wadhifa, heshima wala umuhimu wake kwa jamii. Hizi ni kazi za ibilisi kuanzia yule anayekubali kupigwa picha akiwa uchi mpaka kwa yule anayesambaza na kufurahia. Kwani wapo watu wanaofurahia kupigwa picha wakiwa uchi na wakifurahi picha zao kusambazwa ktk mitandao. Lakini pia fulsa hiyo pia imetumika kama kukomoana miongoni mwetu na hizi ni kazi za Ibilisi zote, na hawa watu wanaofanya hivyo ni agent wa ibilisi.

Hii kuikabili ni ngumu kwa hali ya kawaida bali ni kwa wahusika kujithamini wao kuwa wameumbwa kwa mfano wa Mungu hawatakiwi kuuzalilisha uumbaji wa Mungu. Na wale wanaodhalilisha wenzao kwa kusambaza picha hizi wajue wandhalilisha uumbaji wa Mungu. Wanatakiwa wajirudi waombe rehema mbele za Mungu ili awasamehe na kuacha kabisa biashara hiyo.
 

Pengine hapa tutatofautiana. Mimi naamini hii tabia ya wote kujifanya viranja wa maadili ndiko kulikotufikisha hapa. Kwa nini mambo ya watu binafsi tusiwaachie wenyewe wamaliziane? Kama mtu unamuona ana mienendo mibaya, jitenge naye lakini usimpeleke kwenye jukwaa la umma! Mimi naamini sisi sote, hakuna aliye kamilika sasa kwa nini tuanze kuwahukumu wengine kabla ya kujihukumu wenyewe? What's good for the gander etc. etc. Kama mtu anajiona amekamilika basi heri amshukuru Mungu ili aweze kuendelea hivyo hivyo.
 

Ufunuo,

You bring a very important point about the use of this double edged sword called technology.Kuna rafiki yangu baada ya kuwa addicted na mitandao ya picha ambazo hazisemeki aliapa kutoikaribia computer yenye internet zaidi ya kwa ajili ya kutuma email kwa sababu alishaona internet ni "shetani mkubwa"

Wakati huo huo wengine tunakuja hapa JF na kukata issues za kitaifa, wengine inawasaidia katika homework za shule na research za kazini, wengine inawakeep in touch na familia ndugu jamaa na marafiki.Kwa hiyo internet ni kama moto, unaweza kuutumia kusonga ugali ukala au unaweza kuutumia kuunguza nyumba, shauri yako mwenyewe.

Sasa ukiona mtu anatumia moto kuunguza nyumba that tells you more about the person than about moto.

Bottom line is we have to be careful out there, always associate with good peeps and keep away from dubious characters.And even then, certain exposures are a huge risk if you get my drif.
 
Mkuu Pundit

kwa kuwa JF tunaongea kwa uwazi, naomba uweke wazi jina ra huyo mtu ariyepiga picha na kuzisambaza. Hii ni adhabu ndogo tu compared na kumdharilisha huyo dada.

Naomba kuwakilisha.
 
sijaelewa unazungumzia kina nani hao wasio na heshima

Offcourse hao wanaosambaza huo upuuzi tena bila kuombwa wanadhani watu wote wanapenda kushabikia upumbavu wao. I am sorry i am so touched though sijaona hiyo email thats why nikashindwa kuweka wazi what i mean
 
Pundit you have a very valid concern which I support fully! Lakini bottom line lazima tufikirie mbali zaidi. Pundit, believe me you, huwezi kumbadilisha mtu kwa "maombi" ndo maana haya yoote unayoyasoma na kuyaandika humu wenzetu kwenye nchi zilizoendelea wameshayakubali kama part ya maisha yao. Na sisi ndo tunaiga huko (thanks to google!) Ndo maana Ngono, ufedhuli, hizo night club uchwara,nk ni part ya maisha ya wazungu, precisely kwa sababu walishagundua kwamba si rahisi kuwazuia watu kufanya watakavyo, after all ndo uhuru wenyewe huo (wameshahalalisha umalaya, strippers.. You know better..)

Sasa je nakubaliana na haya mambo? hapana. Kikubwa hapa ni kwamba nchi zetu za kimaskini hatuna budi kuwa na sheria na UWEZO wa kuzitekeleza. Kama tungeinvest katika utekelezaji wa sheria tungeweza kupambana na haya majanga, lakini kwa mwendo huu wa waungwana kama wewe na wengine kusisitiza maadili..no body cares or listens! Dunia imeshabadilika sana. Ulaya hata malaya anaithamini kazi yake na anathaminika! is it the same here in bongo? I dont know! binadamu ni kiumbe tofauti sana na ingawa tuko billion sita na ushee tunatofautiana kila mtu kivyake...

Hili swala ni gumu sana, wengi especially watawala wetu..wanakimbilia katika kivuli cha "maadili ya mwaafrika" This stament is just outdated and full of hypocricy. Kama mtu akifanya mambo kama hayo angekuwa anaweza kuface consequences za sheria..hali ingebadilika. Kifupi, all those vices you see in our country/Africa ni kwa sababu people knows kwamba kuna level katika maisha sheria haiwezi kukugusa.

So we have to identify our commonalities kama bianadamu na tu move on..kuna vitu hata kama ungevipigia kelele..you will hardly succeed! Its sad but you have to do the doables...kuwaomba watu wafuate maadili..its not the nature of human beings. Nani hajui kwamba kuiba ni vibaya? viongozi wanaingia maofisini kwa viapo vya misahafu...Its disguisting, but hili swala la maadili mimi nashindwa kulielewa na kibaya linatumika kwa convinience za mhusika...
 

Vijana wengi tu wana mapicha ya aina hiyo. Tena ukijaribu kuwaelimisha wanakuona hufai na umeachwa na wakati. Na wengine wana CDs maofisini wakati wanachapa kitu kwenye komputa huwa wanaangalia watu wakifanya mapenzi machafu (mfano kinyume na maumbile) na wanaona ni sahihi kabisa.

Yaani, kuna vituko vingi sana katika jamii yetu inayotokana hasa na ujinga tu. Sasa sijui kama ndiyo maendeleo au kurudi nyuma? Kitu kingine sisi tunaotumia usafiri wa daladala tunasikia matusi yakitolewa na madereva, makondakta na mashabiki wao utafikiri hawa watu hawakuzaliwa na wanawake.

Siku moja kondakta mmoja alikuwa akimtukana mama fulani wa makamo hivi mpaka nikaona aibu. Kijana huyo alikuwa akimwambia huyo mama, "Kwani kati yangu na wewe nani mwenye muhogo: mimi, wewe?" Kwa jinsi huyo kijana alivyokuwa akiongea nilielewa alimaanisha 'mzee'. Sasa kweli huu ni ustaraabu kweli? Inabidi tubadilike katika mambo mengi sana: elimu, mtazamo, maadili, kuongea, kufikiri, nk.
 
Pundit, kwa kweli nakushukuru na kukupongeza kwa kuweza kulisema hilo bayana. Nakubaliana kabisa na wewe kwamba pamoja na mapungufu ya wahusika kwani hafanyi hayo mambo peke yake, bado haistahili kuyaweka hadharani ili kila mtu ayaone. Kuna njia nyingi za kuonya watu na si lazima kudhalilishana. Vilevile inawezekana ukafikiri unawakomoa wahusika/mhusika kumbe ukute wala haliwagusi/halimgusi. Matokeo yake unadhalilisha umma mwingine usiostahili.
Kwa wasiokubaliana na Pundit, siwezi kuwalazimisha wawe na maoni kama yake kwani binadamu tuna mitizamo tofauti. Lakini naamini idadi kubwa itakubaliana naye na hasa tukizingatia malezi katika jamii nyingi za kitanzania kwa upande wa mila na desturi na hata dini zetu.
 
Let them forward the email to us halafu tuwatrack then tuwafundishe adabu ili siku nyingine wasifanye utoto huo hasa hao wasiofanyakazi walizoajiriwa nazo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…