#COVID19 Hivi tunapambana na COVID-19 kweli au tunahitaji mikopo tu?

#COVID19 Hivi tunapambana na COVID-19 kweli au tunahitaji mikopo tu?

LICHADI

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
4,491
Reaction score
12,560
Limepita basi la mwendokasi hapa watu wamejaa kupitiliza yaaani wamebanana humo ndani hatari, ikumbukwe miezi karibia mitatu imepita wameleta basi mpya 70 wazilaza hazifanyi kazi

Hapo hapo wanakwambia tujikinge na corona.

Hii Serikali sijui kama ipo makini kweli or tunapambana ili tupewe mikopo.

Na ndio maana hata hizi chanjo tunakuwa na mashaka nazo either zipo kwa ajili ya kutulinda or tuonekane tumo kwenye ramani ya dunia tupate mikopo

Maana nyuma ya pazia sehem hatarishi ambazo watu wanaweza kumwagiana huu ugonjwa ni kwenye vyombo vya usafiri hasa mwendokasi ambapo watu wanajazana maana magari machache.

But Serikali haionyeshi kama wapo serious kweli, huwezi laza gari 70 ukaacha gari chache zitumike ukijua kwamba upo ugonjwa hatarishi ambao unasambaa kupitia misongamano.
 
Limepita basi la mwendokasi hapa watu wamejaa kupitiliza yaaani wamebanana humo ndani hatari, ikumbukwe miezi karibia mitatu imepita wameleta basi mpya 70 wazilaza hazifanyi kazi...
Kwa vile hakuna mpango mikakati wowote unaofahamika wa kupambana na huu ugonjwa basi mwendo ni kodi, tozo, mikopo na misaada.

Zinatakiwa njuluku!
 
Tunaishi kimungumungu na kubahatishabahatisha na mambo yanaenda. Tutavuka tu kwa uwezo wa Mungu. Bila kudra za Mungu wote tungeangamia zamani sana. Kipindupindu tu kimeshindwa kutufyeka ije iwe iyo Corona?
 
Vile Corona inaringa Tanzania![emoji16][emoji16][emoji16]
2226502.jpg
 
Sisi wazalendo tukisema korona haipo mnatuona mianga & vimbwanga wa Ruangwa 🙂
 
Eti wanasema wanakimbiza mwenge ili kumchoma kirusi corona
 
Ni hela tu inatafutwa ndugu, sasa kama wenyewe wanasema chanjo yenyewe haizuii kupata corona ya kazi gani tena. Wamekuja na porojo eti hata ukipata haitakuwa na makali, yaani vitu vya kuchekesha kabisa.
 
Binafsi mimi naona mnahangaika tu Mungu alishatulinda siku nyingi basi tu sisi wenyewe!
 
Watu humu pamoja na magazeti wanatoa shuhuda kuwa Moshi,Arusha na kwingineko watu wanateketea halafu unatamba kuwa ni ugonjwa wa kwenye media?!
Mimi nipo Arusha na mizunguko yangu ni USA River mpaka Moshi, kwa ninayoyaona sasa hivi inafikirisha sana...mwanzoni wa mwaka tulipigwa na nilijiaminisha kwamba ile dhoruba haitakaa ijirudie tena lakini sasa hivi imefunika, kuna baadhi ya sehemu huvuki nyumba mbili/tatu utakutana na msiba na watu wamejaa tu, wengine unakuta ni msiba raundi ya pili ama ya tatu yaani nyumba hiyo hiyo imerudiwa ndani ya mwezi mmoja !
 
kila siku nasikia wanatangaza marathon mara Tanga, Mbeya pia sijaona wakifatilia maagizo yao ya kutaka kwenye mabasi watu wakae level seat na kuvaa barakoa kwa kifupi ni full maigizo
 
Wanaokufa kwa korona Tanzania wanajua wenyewe walichomkosea mwenyezi mungu
 
Watu humu pamoja na magazeti wanatoa shuhuda kuwa Moshi,Arusha na kwingineko watu wanateketea halafu unatamba kuwa ni ugonjwa wa kwenye media?!
Lini walikuwa hawafi huko Moshi? Kwanini ugonjwa uje baada ya kifo cha hayati?
 
Watu humu pamoja na magazeti wanatoa shuhuda kuwa Moshi,Arusha na kwingineko watu wanateketea halafu unatamba kuwa ni ugonjwa wa kwenye media?!
Sikupingi ila ushajiuliza kwanini hizo sehemu ndio watu wawe wanakufa sana?
 
Back
Top Bottom