Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Msumbiji(1977-1992). Tanzania ilikuwa ikiwaunga mkono wajamaa wenzao FRELIMO dhidi ya RENAMO. Kawaida tulikuwa tukiaminishwa kuwa RENAMO ni waovu wasiofaa, lakini mtu kadri unavyokuwa na kupata habari zaidi unaelewa kuwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe huwa hakuna mbaya wala mzuri.
Sasa basi vita ilipokolea RENAMO wakapropose nchi igawanywe, wao waunde jamuhuri ya Rombesia kaskazini na magharibi mwa nchi. RENAMO wana mizizi sana kaskazini wakati FRELIMO wako sana kusini. Mpango huo haukufanikiwa.
Sasa nawaza iwapo tungewaunga mkono RENAMO na hiyo jamhuri ingeundwa si lingekuwa jambo la manufaa sana, hii nchi ingekuwa imebase sana kwetu tofauti na Msumbiji ya sasa iliyobase zaidi South Africa. Hatuna ushirikiano wowote wa maana na Msumbiji, Maputo ipo kilomita zaidi ya 2,000 kutoka Mtwara. Ingekuwepo Rombesia si hata umeme wa Cabora Bassa wangetuuzia? (kwa sasa wanauza South). Pia hawa jamaa wa kaskazini tunashare nao sana utamaduni, kuna Wamakua na Wamakonde huko.
Hata kitendo cha magaidi kuibuka kaskazini ya Msumbiji ni zao la jinsi eneo hilo lisivyojaliwa na Maputo, serikali iliyo zaidi ya km 1500. Kungekuwa na taifa hapo si kungekuwa stable?!
Je nchi hiyo ingeundwa, kungekuwa na faida kwetu?