Wakuu,
Ninavyofahamu mimi mwanamke anazaliwa bikira, akikua akaolewa na au kufanya mapenzi basi ubikira huwa umekwisha pale.
Lakini mbona Mary mama yake Jesus bado tunamuita bikira wakati aliolewa na kuzaa watoto na mumewake Joseph (achilia mbali Yesu ).
Naomba mawazo yenu yasiyo yakishabiki wa kidini, hili swala linanitatiza kidogo
Suhala la Maryam kuendelea kuitwa Bikira Maria ni la kiimani zaidi, na haswa kwa waumini wa Kikatoliki na Orthodox, wao wanasema kuwa
Mary - "ever-virgin" Hii ni kwa sababu Maryam alizaa mtoto wake wa kwanza kabla ya kukutana kimwili na mumewe Joseph.
Japokuwa kwenye agano jipya, Maryam Mama yake na Nabii Yesu, imeandikwa kuwa alikuwa na watoto wengine zaidi (Wakiume na wa kike). Ukisoma Injili kama ilivyo andikwa na Mathayo 13:55-56
Utakutana na maneno haya:
"...Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda?
Na maumbu yake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote?"
Vile vile kwenye Injili kama ilivyo andikwa na Marko, imeandikwa hivi:
Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni?
Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake. (Umbu ni dada)
Marko 6:03
Wakatoliki wanapinga suhala hili kwa nguvu zote nao wanatumia mistari kutoka
Mathayo 27:56, ambayo inasema hivi:
Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yusufu, na mama yao wana wa Zebedayo.
Vile vile wana-quote mstari kutoka
Marko 15:40, ambao unasema hivi:
Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na Salome;
Wanachambua mistari hii kwa kusema kuwa hao watoto ni wa Maryam mwingine na si mama yake na Nabii Yesu. Inasemekana huyo Maryam mwingie ni Binamu yake na Bikira Maria au Wifi yake, yaani dada yake na Joseph.
Vile vile wanawa-quote mababa wakubwa kabisa wa kanisa, wa enzi hizo kina
Clement wa Alexandria,
Origen, na
Mtakatifu Jerome, kuwa waliamini kuwa
Mary was ever-virgin. Vile vile wanasema kuwa hata wakubwa wa KiProtestants kama
Luther,
Calvin,
Zwingli, na
John Wesley, Wanakubaliana na dhana ya Ubikira wa Maryam mpaka kifo chake, na mwisho kupaa mbinguni kuungana na Mwanaye Yesu Kristo.
Ukisoma
Catechism of the Catholic Church, Ukurasa wa 112, saifa ya 499 imeandikwa hivi:
Mary -- "ever-virgin"
499
The deepening of faith in the virginal motherhood led the Church to confess Mary's real and perpetual virginity even in the act of giving birth to the Son of God made man.154 In fact, Christ's birth "did not diminish his mother's virginal integrity but sanctified it."155 And so the liturgy of the Church celebrates Mary as Aeiparthenos, the "Ever-virgin".156
p.112