sorry natoka nje mada kidogo >> Elimu yetu ya tanzania inawalakini mwingi sana kubwa zaidi haipo updated ... iam sure lile daftari langu la physics la advance leval nililomuachia rafiki yangu basi alimpatia mdogo wake.. na mdogo wake akampa rafiki yake.. wakisoma material yaleyale.
hapa nilikuwa nasoma makala ya BBC (
BBC Swahili - Habari - Vyuo Vikuu Afrika havitambuliwi )
kuna mahala wacha ni quote wameongea ukweli mtupu ..
nikweli ukiangalia wanafunzi wengi sasa hivi wanakimbilia India, china, malaysia, philipines, rusia, romania ... etc ..
mwandishi akaongezea ...
nikirudi kwenye mada hayo yaliwahi kunikuta mimi wiki moja kabla ya mtihani wangu wa A-leval mwalimu alitunga mtihani wa chemistry mgumu sana, nakumbuka nilipata 2% ulemtihani.. ilikuwa si kawaida kwa shule kama mzumbe mtu wa kwanza chemistry kupata 20%.. alafu akawa anatudhihaki kwamba .. hamsomi... wiki kabla ya mtihani mnapata matokeo kama haya.. sitokuja kumsahau yule mwalimu... alitakiwa atutayarishe kisaikolojia kuwa ready kwa mtihani yeye alitu discourage.. na kutaka tupoteze matumaini kabisa "hao ndio walimu wetu" wanaona sifa akiambiwa katika mtihani wa taifa hakuna mwanafunzi aliyeweza kujibu swali lako. "upuuzi m2pu"
binafsi mimi kabla ya kupata schollership na kuja kusoma huku ughaibuni nilianza kusoma pale muhimbili .. kilichonikimbiza . muhimbili badala ya kukutayarisha kuwa dactari... wanakutungia mtihani ili ufeli!! hii ni tofauti kubwa sana kati ya vyuo vyetu vya serikali na vya huku mbelembele...