Waliotangulia wamekujibu vizuri sana, kazi ya mbunge si kuwakilisha chama bungeni, anawakilisha wananchi waliomchagua na kuisimamia serikali kwa manufaa ya taifa. ZZK anweza kuifanya hiyo kazi vizuri bila msaada wa CDM, ngoja katiba mpya ianze kufanya kazi nadhani hata haya mambo ya kufukuzana hayatakuwa na maana tena.
Lakini kama Great thinker ulitakiwa pia kujiuliza, utafanyaje iwapo watu wachache ndani ya chama wamefanya Lobbying ili ufukuzwe uanachama kwa masilahi yao binafsi, je utakaa kimya haki yako ipotee? Kama una ushahidi kuwa ZZK ni msaliti leta hapa janvini na siyo kuendekeza majungu kwa kutumia waraka ya kumchafua ZZK ulioandaliwa na CDM. Mbona suala la Mbowe kuchukua hela kwa Mkono haujauliza, huyo si msaliti? Kwa nini akachukue hela kwa mtu ambae chama kilimtaja kama fisadi? Hapo usafi wa Mbowe uko wapi?