hIVI UBUNGE WA MAHAKAMA UNA RAHA GANI KAMA UMEKATALIWA NA CHAMA?

amakyasya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
3,480
Reaction score
914
Ukishajua kuwa chama hakikutaki hata kidogo kwa kukuchoka kwa kukiuka matakwa ya chama halafu unang'ang'ania hadi mahakamani, kuna raha gani ya kuwa mwanachama kwa amri ya mahakama? Hii inatokana na mfano halisi kwa Zitto Kabwe na wengineo wa aina yake.
 
Maana ya ubunge ni kuwawakilisha wananchi wa jimbo(constituency) husika kwa maendeleo ya taifa na Siyo chama au nimekosea?
 
raha yake ni kwamba unaendelea kuwakilisha wananch waliokuamini na kukuchagua na kupata manufaa yote kama mbunge. C lazma chama ndo maana hata wagombea binafsi wapo sehem nyngne na wanapga kaz bila vyama
 
Maana ya ubunge ni kuwawakilisha wananchi wa jimbo(constituency) husika kwa maendeleo ya taifa na Siyo chama au nimekosea?
Lakini kumbuka kuwa mbunge anatokana na chama kilichompitisha ili agombee. Sasa mbunge anapoasi chama kilichompa ticket ya kugombea inakuwaje mkuu?
 
Mkuu

Hawa hapa wanashndwa tu kusoma alama za nyakati pia usaliti unawapa tabu sana yaani undumilakuwili

Zito KabweHamadi RashidiDavid Kafulila

Nadhani wanaweza kutupatia majibu mazuri lakini kwa mtazamo wangu bora wangekubali tu kutemwa yaishe haya mambo maana kama chama unakipenda kwanini ufanye usaliti halafu uwahi mahakamani ?
 
raha yake ni kwamba unaendelea kuwakilisha wananch waliokuamini na kukuchagua na kupata manufaa yote kama mbunge. C lazma chama ndo maana hata wagombea binafsi wapo sehem nyngne na wanapga kaz bila vyama
Kwa hiyo unamshauri Zitto awe mgombea binafsi kwa uchaguzi mkuu ujao? Maana CHADEMA hawamtaki! Labda aende CCM.
 
wanasayansi ya jamii wanasema "Knoledge is not universal". Hapa naona kuna tofauti kubwa sana ya neno USALITI lakn binafsi nadhani neno hili linatumiwa kama kisingizio tu na baadh ya watu ili kuwabagua wengne!
 
Kwa hiyo unamshauri Zitto awe mgombea binafsi kwa uchaguzi mkuu ujao? Maana CHADEMA hawamtaki! Labda aende CCM.

maana yangu ni kwamba anaweza kuwakilisha wananch wake hata kama ni mbunge wa mahakama
 
Maana ya ubunge ni kuwawakilisha wananchi wa jimbo(constituency) husika kwa maendeleo ya taifa na Siyo chama au nimekosea?

Hiyo hapo kwenye blue, ingependeza sana kama ingekuwepo kwenye katiba mpya.
Namaanisha kama katiba mpya ingeruhusu watu kuwa viongozi bila ya kupitia kwenye chama cha siasa.
Hapo tungepata viongozi halisi na sio kama hawa tulionao sasa.
Hivi sasa viongozi wajali maslahi ya vyama vyao zaidi kuliko maslahi ya wananchi na taifa.
 
Alichaguliwa na wananchi wa kigoma kasakazini na sio chama acha UJUHA wa MFALME JUHA
 
Uko sahihi mkuu. Chukua likes mia.
 
maana yangu ni kwamba anaweza kuwakilisha wananch wake hata kama ni mbunge wa mahakama

Hakika anaweza kufanya hivyo, ila katiba ya sasa hairuhusu hayo.
Mbunge lazima atokane na chama cha siasa.
Hapo ndipo kwenye changamoto, itabidi kwenye katiba mpya tukubali kuwa na wagombea binafsi.
 
SAHIHISHO: Vyama ni vehicle tu la kukupa ubunge; Ubunge unapewa na Wananchi na Unahudumia wananchi sio chama!
 
Lakini kumbuka kuwa mbunge anatokana na chama kilichompitisha ili agombee. Sasa mbunge anapoasi chama kilichompa ticket ya kugombea inakuwaje mkuu?

Kamuulize JUNIOUR SLAA BABU
 
Alichaguliwa na wananchi wa kigoma kasakazini na sio chama acha UJUHA wa MFALME JUHA

Sasa mbona unaweka ujuha wako peupe kiasi hicho, kwani Zitto hakupitia chama chochote kugombea ubunge hadi kuchaguliwa na wananchi wa kigoma kaskazini?
 
Zzk hata akiwa mgombea binafsi hawez kuwa rais labda kigoma iwe nchi.kwa mtazamo wangu kuna vyama vinamsifu kwa unafiki tu zzk na wengine kuwa wabunge wa mahakama coz uanachama wa chama haupatikani mahakamani.maybe shetan atamlipa ujira wake zzk si muda mrefu ikibidi amchukue!
 
hatuzungumzii urais hapa toa masabuli yako
 
Waliotangulia wamekujibu vizuri sana, kazi ya mbunge si kuwakilisha chama bungeni, anawakilisha wananchi waliomchagua na kuisimamia serikali kwa manufaa ya taifa. ZZK anweza kuifanya hiyo kazi vizuri bila msaada wa CDM, ngoja katiba mpya ianze kufanya kazi nadhani hata haya mambo ya kufukuzana hayatakuwa na maana tena.

Lakini kama Great thinker ulitakiwa pia kujiuliza, utafanyaje iwapo watu wachache ndani ya chama wamefanya Lobbying ili ufukuzwe uanachama kwa masilahi yao binafsi, je utakaa kimya haki yako ipotee? Kama una ushahidi kuwa ZZK ni msaliti leta hapa janvini na siyo kuendekeza majungu kwa kutumia waraka ya kumchafua ZZK ulioandaliwa na CDM. Mbona suala la Mbowe kuchukua hela kwa Mkono haujauliza, huyo si msaliti? Kwa nini akachukue hela kwa mtu ambae chama kilimtaja kama fisadi? Hapo usafi wa Mbowe uko wapi?
 
Anajadiliwa nani hapa! Ooops! Ni yule Mbunge wa Mahakama kwa tiketi ya CCM! Ahesabu ameumia! Akawaulize waliorudishwa kinguvu na Mahakama katika ndoa zao, kama wanazifurahia tena!
 
Kumbe unajua kuwa mgombea binafsi hadi katiba mpya kwa maana hiyo kwa sasa mbunge ni lazima apitie chama cha siasa ndipo achaguliwe na wananchi kuwawakilisha bungeni!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…