Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Wakuu, mimi ni mkazi wa Tandika Mwembeyanga jijini DSM, mara kadhaa nimewaona wadada na wamama wa huku Tandika wale ambao ni wajawazito wakihaha kutafuta udongo ambao huutumia kama chakula, ningependa kufahamu faida wanazozipata kwa kula udongo huo ambao huuzwa kwenye magenge kadhaa kwenye eneo letu.
Kwa kadiri ya ufahamu wangu, udongo zaidi ya kuleta uchafu labda na minyoo kwenye mwili wa mtu sioni kingine ambacho mtumiaji anaweza kukipata, sasa labda kama kuna anayefahamu basi anijulishe faida wapatazo wanawake waja wazito wanaoutumia udongo kama chakula.