Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
nimesoma uzi mmoja humu unaelezea kwamba nchi hizi ziumeungana katika ulinzi, yaani ukivamia mmoja umevamia wote. wengi wamechangia kwamba ni mbinu ya kagame kutaka kuvamia tanzania lakini mimi nina swali najiuliza. ukiangalia kwa makini nchi zote hizi ziko katika bonde la mto nile na zina hamu kubwa ya kutumia maji ya mto nile. hasa kenya ambayo inataka kufanya irrigation kutoka ziwa victoria na ethiopia ambayo inakabiliwa na njaa na inataka kufanya irrigation huku ikijenga hydrodam kubwa kabisa africa. rwanda, uganda na sudan kusini zina hamu kubwa ya kutumia mto huo. misri wako tayari na mgogoro na ethiopia kuhusu ujenzi wa bwawa hilo na rais morsi alisema hata sita kwenda vitani. pia tukumbuke kuwa nchi zote hizi tano zinakinyongo na misri kuhusu maji ya nile na pia inatabiriwa kuwa huko tuuendako vita nyingi vita zitapiganwa kugombea maji. swali ni je hawa watano wana adui gani in common hadi wamuundie alliance?, je nchi hizi inajiandaa kupigana na misri ambaye ni africa supepower?