Wanajamvi,
Naomba mwongozo hapa. Nimesoma mara kadhaa kwenye magazeti na mitandao ya kijamii kuwa watu wamefumaniwa na wamepelekwa polisi kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka. Naomba niulize maswali yafuatayo;
1. nafunguliwa mashtaka kwa kosa lipi, wizi, unyang'anyi, udhalilishaji au ubakaji?
2. Sheria gani hua inatumika kutoa hukumu kwa mtu aliyefumaniwa na mke/mume wa mwenzake?
3. Kesi za namna hii huwekwa kwenye kundi lipi? Ni kesi ya jinai, madai au mauaji na zinginezo?
Msaada kwa waelewa wa mambo!
#MasaiWaKinyakyusa .
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums