Hivi ukimuondoa Harry Kane, England hawana World Class Player mwingine, Wanaenda kutembea tu Russia

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Leo tujadilini timu ya media. Timu ya Taifa ya England au maarufu kama The three lions wamefuzu na watakuwepo katika fainali za Kombe la Dunia pale Urusi mapema June 2018.

Ukiangalia Wachezaji wanaounda kikosi chao, unaweza ukasikitika kama sio kusononeka. Nyota wa timu ni Harry Kane, nakubali anajua kufunga, je akina nani wapo nyuma yake katika timu ndio habari ya kubwa.

Leo hii walinda milango wao ni wa kawaida sana, Joe Hart ametolewa kwa mkopo West Ham na anakaa benchi. Golikipa mwingine Jack Butland timu yake imeshuka daraja na hajawahi kushiriki hata Europa Ligi.

Ukija mabeki, kuna akina John Stones, Smalling ambaye wote mnajua anavyobabaika, kuna beki tegemeo wa kushoto Ashley Young, what a joke! atleast Kyle Walker ananishawishi na yule Harry Maguire wa Leicester.

Kwenye kiungo, kuna Henderson kiungo anayejua kupiga square pass, kuna akina Eric Dier, Wilshere ambaye hayupo fomu ila lazma aitwe, pia kuna Dele Alli ambaye wote ninyi ni mashahidi amekuwa na fomu ya chini sana msimu huu unaoisha kesho.

Mimi nathubutu kusema, England kwa aina ya wachezaji walionao akivuka kundi lake atakuwa amejitahidi sana! Vinginevyo nieatakie safari njema ya utalii wao ndani ya Russia.

Povu ruksa!!
 
Binafsi sijawahi kuwaamini waingereza toka nianze kushabikia mpira.. Kama wilshere atakuwa katika form nzuri atakuwa msaada mkubwa kwao.

Wakati mwingine katika soka bahati inahitajika kwa kiasi kikubwa mkuu, timu si lazima iwe na wachezaji wa kiwango cha dunia wote, m1 anatosha sana na hawa wengine wa kawaida kama watajituma, kujitoa kwa ajili ya timu plus maelezo na mbinu bora za kocha.
 
Hivi kombe la dunia lililopita Columbia alikuwa world class players wangapi ?
 
Wapange tu hivi
1. Butland
2. Alexander anord
3. Ashley young
4. John stone
5. Cahill
6. Jonjo/milner
7. Sterling
8. Handerson
9. Crouch
10. Kane
11. Rashford
 
Kipa si wamchukue huyu wa Bunley i
NICK POPE maaana jamaa anajituma sana
Naunga mkono hoja, dogo amepewa nafasi mara baada ya kuumia kwa mlinda mlango wao namba 1 klabuni Burnley ila toka hapo amekuwa na msimu mzuri na kwangu mimi naona angepewa nafasi walau awepo kikosini kuelekea Russia.

Ila Southgate atawabeba Hart, Butland na Pickford.
 
Kweli we ndugu una bifu kali sana na Uingereza!!!!!!

Liverpool amekwenda fainali ya UEFA with some stunning performances of British midfield trio ya Jordan Henderson, James Milner and Alex oxlade Chamberlain.

Left back best performances of Fabien Delph after Benjamin Mendy suffered a serious injury. John Stones,Chris Smalling,Phil Jones,Michael Keane,Gary Cahill,Ryan Bertrand are wolrd class.

Check Eric Dier pale kwenye midfield, ongezea zile attacking talents za Raheem Sterling,Delle Alli,Jesse Lingard huku mnyama Harry Kane akifanya yake with deadly kid Marcus Rashford waiting at the bench while the predator Jamie Vardy hunting a thief in the dark.

My friend,patachimbika Russia
 
Henderson huyu anayepiga square pass muda mwingi wa mchezo. Milner ameshastaafu timu ya taifa. Chamberlain ameumia atakosa michuano.

Mabeki ulionitajia kua ni world class players bado kidogo nivunje glass kwa kucheka. hivi smalling nae world class player? mkuu wewe endelea kuipenda timu yako ya uingereza tu, maana ushalishwa unga wa ndere.
 
Dogo anaokoa hatari nyingi sana pale Banley yaani sawa na De Gea anavyowabeba Manure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…