Hivi ukoje?

Hivi ukoje?

Davety

Member
Joined
Dec 14, 2018
Posts
76
Reaction score
70
Wanazengo mpo?
Ase hivi kuna umri ukifika unakuwa hauna yule close friend hasa kwa sisi wanaume au ni Mimi binafsi??? Kuna umri ule ambao ukiwa bado bachela hauna familia unakuwa na wana mda wote mnaiva story sana

Lakini kwanini ukishaoa na kuwa na familia tu marafiki kikawaida hupungua inabaki marafiki zako wale wa mwanzo kama watu wengine tu.

Mimi pia sina rafiki yani yule very close friend wote ni kama watu wa kawaida tu na niliamua kufanya hivo baada ya kuona marafiki wengi nilionao niwatu wakunirudisha nyuma kimaendeleo

Rafiki unamkopa pesa harudishi ukimpigia simu hapokei mipango yako inaharibika hao ni marafiki kweli?ikafika mahari nikaona niwe kivyangu vyangu.

Kwangu mm sina rafiki yule ambae wakaribu sana mpk huwa nahisi au nakosea mahari?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom