Nasubiri..
Hata wazungu wana uchawi wao sema sio wa kimaskini kama sisi waafrika.
Wenzetu wameipa kipaumbele elimu na maarifa ndo mana ni ngumu kukuta wanashikana mashati eti mzee wattson na mkewe wanamroga mzee Floyd ili asipate kazi serikalini
Wanalima mashamba kwa teknolojia za kisasa,wanazingatia mbolea,madawa,majira nk!
Hata akikosea atafanyanutafiti atagundua dawa alizouziwa hazikua sahihi ndo mana mazao hayajastawi yamedumaa...ila sasa itokee tz hapo mzee mwaipopo kashaanza kuzipanga na mzee tuntufye anadai anamroga viazi vyake visiote,kaambiwa na mganga kumbe kauziwa mbegu mbaya [emoji1][emoji1]
Mtu una insomnia unadai wanga wanakuchezea usilale.
Una typhoid unatapika na kuharisha,hospital wanakwambia una Uti na malaria.unatumia dawa hazisaidii unakimbilia kwa mganga nimerogwaa!
Mifano ni mingi tu.ila ushirikina umekua mkubwa africa sababu ya elimu duni na ukosefu wa maarifa!