Hivi ulishawahi kuishi kwa kudra za washikaji, haya maisha yasikie tu

Hivi ulishawahi kuishi kwa kudra za washikaji, haya maisha yasikie tu

Teslarati

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2019
Posts
2,621
Reaction score
10,466
Miaka ya zamani kdg ndo nimemaliza chuo nikapata kazi kwenye NGO moja hv. Huko nikawa naponda sana mali, yaani ilikua ni gambe na mademu tu. Mara paaa NGO ikamaliza issue zake wakafunga virago, nikabaki sina kazi na hapo nilikua nimempa mimba binti mmoja hivi na ndo ilikua mimba ya mtoto wangu wa kwanza.

Maisha yakawa magumu kinoma, kupata kazi shida, nilizunguka kinoma hadi vibalance vikaisha, home mm ndo wananitegemea kwa hio nisingeweza kuomba hela huko.

Kilichofuata sasa niliishi miezi mitano bila kazi lkn kwa kudra za washikaji, yaan leo unaomba huku, kesho kule, keshokutws unarudi kule mwanzo, ni shida tupu. Hadi yule binti anajifungua nilikopa hela ya hospital ila mshikaji alonipa akanambia nisiirudishe.

Washikaji ni zaidi ya ndugu, ishi nao vzr.

Nimekumbuka hii story sababu kuna jamaa mmoja ana familia yake naona alipitia kitu kama nlichopitia mm kuhusu kazi, nilihamia hapa nikamkuta, wote tumepanga nyumba kwenye fence mona ila ghafla jamaa asbh namuona kwake, nikirudi mchana namkuta, jion namkuta pia. Nikahisi yupo likizo, sasa miezi miwili nyuma akanifuata akanielezea changamoto zake anazopitia akaomba nimkopeshe milion kadhaa, nikamkatalia ila nikamwambia labda nikutafutie kazi.

Sasa kipindi namtafutia kazi akanicheki tena akasema anadaiwa kodi na hata msosi anasua sua kuhudumia home, mm nikasema isiwe kesi, nikamchangia 500k huku naendelea kumchekia kazi. Wiki 2 baadae jamaa akapata kazi ila sio nlokua namtafutia, akaitwa kwenye interview dodoma, akawa hana nauli, nikampa 200k akaenda na wala hakuwahi kunipa majibu kama alifanikiwa au la, ila mm sikujali.

Juzi jamaa karudi pale hata hakuja kunipa salamu kama alivyokua anakuja kulialia shida, leo nimeamka na hangover sijaenda kazini naona jamaa asbh kaleta pickup ina namba za DFPA (probably kapata kazi) anahamisha vitu. Ile natoka nikamuona ndo akapata sijui aibu eti anakuja kunisalimia mara "Bro samahani sana mambo yalikua mengi sana" mie nipo kimya tu, aliponiuzi anasema eti "nikiwa free nitakucheki tuje tuongee vzr ila interview nilifanikiwa", nikasema poa lkn akilini nikasema huyu taahira aombee asije kupata shida tena, maana hajui kuishi na watu.

Sio lazima utoe shukran, lkn kuwa na ustaarabu wa kusaidiwa na kuwa na 'honour' kwa washikaji.

Honour unayowapa washikaji wako ndio itakubeba wewe, bila honour watu watakudharau na hautosaidika hata wakukute unakula nyasi na hela wanakuwa nazo za kuhonga na kunywa gambe. Be honarable.
 
Hugo gujamaa kwanza ni gusinitch na pia gujinga sana .
Marafiki ni watu fulani ukibahatika kuwapata watakushangaza sana na pia ni watu ambao hautatamani kuwapoteza shida uwa ni kuwapata wa aina hiyo .

Nishapata majanga Ila mwanangu mmoja alisimama na Mimi wakati kelele za wengine zikiwa nyingi alipambana mpaka nikawa huru ,hivyo Wana wapo na bado wanaishi .

Yaani mshikaji anakusaidia unatamani unavyomshukuru useme nakupenda sana mwanangu Ila unaogopa atakuhisi vibaya inaishia kusema nakubali mwamba ,yaani wewe acha
 
Nilipitia hali kama hiyo kipindi nimemaliza chuo 2012 hiyo, huyo mama mwenye nyumba ana roho ya dhahabu, niliishi kwake bila kulipa kodi, nilipo pata kazi mkoa mwingine nika mtumia pesa yote. Napotezaga namba zote ila ya huyu mama kamwe siipotezi, kuna jamaa zangu wawili walinipambania sana kunitafutia kazi, duh sitawasahau mpaka kesho
 
Washkaji ni watu sanq wanangu tuishi vizur na marafiki. Japo wengine miyeyusho ila mkiishi vizur siku mnakuja kutoana katika maisha.!

Kuna mshkaji wangu nilimueleza shida yangu akaitikia ila akanikaushia kama miaka miwili hivi kimya

Siku from no where akaniambia tuma cv yako kijana kuna sehemu nikuchomeke

Dah mungu amuweke huyu jamaa mpaka Leo namuombea dua njema

Familia yangu yote wanamuombea dua nene.
 
Back
Top Bottom