Hivi ulishawahi kuishi kwa kudra za washikaji, haya maisha yasikie tu

Wengine tumeishia kuwa na wana masnitch ambao tuliwabeba kwa mikono miwili...roho zetu nyeupe zinapata malipo ya maumivu kutufanya tuanze kuwa makauzu.
 
Jitahidi ummpe appreciation zake mwenyewe kwa kusikia kadri uwezavyo.
 
Kuna mtoto nimemsomesha,nimeshuka kiuchumi kwaajili yake,kaanza kulipwa tangu yupo chuo,leo kapata kazi nzuri anaishi apartment na wazungu ananisema kwa watu kua sijielewi,nimekosea maisha..wakati sijawahi kumuomba hata Vocha..

Saikolojia ipo hivi,ukimfanyia mtu wema mkubwa Sana ambao kivyovyote hawezi kukulipa,atakulipa ubaya tu,anaogopa akiwa cool nawewe always atakua mdogo kwako,nayeye kashajipata kwanini umuone kama masikini??

EGO IS THE ENEMY..

Nilisoma kitabu kinazungumzia

Adopted children who kill their adoptive parents..​

Interview watoto walioasiliwa ambao wameua wazazi walio was adopt..visa hivyo vipo vingi Sana...
 
Umeandika point moja kubwa sana
 
Pole sana kaka.....kama mambo yako yanaenda endelea na maisha yako usijisumbue nae...siku akijaa kwenye mfumo unampa vidonge vyake.
 
Mkuu, hongera sana kwa kuwa na moyo mweupe kama maziwa.na amini kuwa hutakuja lala na njaa hata siku moja na ikitokea Mungu atakuwa na kusudi lake.
Waungwana hunena kuwa binadamu sio wabaya bali binadamu wenzao ndio huwafanya kuwa wabaya.
 
Veru touching, thanks
 
Hao shetani amewaweka wakfu ili waondoe huo mtindo wa upendo wa kupigana jerk. Hongera Kwa uelewa mpana ila usiingie Kwenye jaribio la kugoma kusaidia wahitaji wa kweli. Hapo Hola ya Mwovu itakuwa imeua ndege wawili Kwa jiwe Moja. Hopefully you get me point.
 
Mpwa wangu nimempiga sana Dafu akiwa chuo Hadi amemaliza Chuo Mimi nimesaidia sana Masomo yake lakini Tangu apate ajira ,,ananiona ni mtu niliefeli maisha
Mwezi uliopita alitaka aniweke ndani nilimkopa nilichelewa kumlipa Kama siku tatu eeh nusura aliweke Rumande . Nimelalamika sana..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…