Hivi unajua unakatwa 10% na CRDB kila unatumia kadi yako ya kulipa kwa dola?

Bakulutu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2011
Posts
2,557
Reaction score
1,787
Kama ulikuwa hujui CRDB wanakukata 10% kwa kila unapolipa kwa Dola ($) kutoka account yako ya Tsh. Mfano juzi nimelipia 216$ nilikuwa na salio la Tsh. 618,591.67 mwisho nimebaki na 75,993.47.

Japo wanadai hata mabenki mengine ndio hivyo hivyo.

Hii sio sawa kabisa 10% ni kubwa sana asee kwa uchumi wetu.

 
Daah! Hatari! Umekatwa takribani 88,000 kwa transfer ya 520,000?? Duh! Huu wizi!

Hapo wamenipasua rate (2570 x216) +10% ambayo wamechukua zaidi 50478.2 badala ya 555120 kama kusingekuwa na hizo chaji [emoji35]
 
Sasa SI Bora utumie visa ya mpesa?
 
We nawe mjinga. Fungua acc ya dola ndio uwe unafanyia malipo ya dola. Tena nakushauri uende stanbic wana account inaitwa personal current acc ina card ya gold.. haina makato na ni iko poa sana kwenye online payments!

Tzs acha crdb ukitaka dola badilisha then peleka kwenye account ya stanbic
 
Kwanini usinunue dola ndo ulipe au usilipe Kwa madafu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…