Hivi unaweza kuwa na akili timamu ukakubali baba yako mzazi auze samaki akiwa na umri wa miaka 92 na ukakubali alalie mkeka?

Endelea kuchezea haki za wanao ukitarajia huruma zao ukizeeka eti mzazi hakosei.

Karma ipo ndugu
Haki Kubwa Zaidi Ni Ile Mimi Kukufanya Uwe Hapa Duniani Ukivuta Oxgern
Mengine Ni Wajibu Tu.
Ni Sawa Na Mtoto Aliyezaliwa Na Wazazi Masikini Na Walioshindwa Kumpa Matunzo Alafu Baadae Mtoto Awe Tajiri Alafu Aseme Simsaidii Baba Angu Sababu Yeye Alikuwa Mvivu Na Alishindwa Kunisaidia Na Kupambana Kwa Ajili Yangu.
Kila Mtu Ana Njia Zake Hapa Duniani
Cheo Cha Mzazi Ni Kikubwa Sana Ukitumia Akili Yako
Na Ukiona Una Chembe Chembe Za Kuona Mzazi Anakosea Haupo Mbali Sana Na Kuona Hata Mungu Kuna Vitu Nae Anazingua.
 
Mzazi Akosei.
Sasa Watoto Umewazaa Wa Nini?
Kwa Mujibu Wa Uislamu
Watoto Na Mali Zao Vyote Ni Mali Ya Baba.
Haujawazaa watoto wakuhudumie au wakulee. Baba au mama tengeneza maisha ambayo hutakuja kuwasumbua watoto wako.
Dini ndiyo msingi wa umasikini na kuendekeza mila potofu. Watoto ni nafsi huru zinazojitegemea na kuwazaa siyo kigezo cha wao kukuhudumia. Mzazi akosei? nani alikudanganya? Amka
Hao watoto wanafamilia zao, wanatakiwa wahudumie familia zao na siyo wewe.
 
Kama mzazi hakosei basi hana dhambi. Dini na tamaduni za kiafrika ndizo zimewafanya waafrika tumekuwa kwenye kuamini mambo ya kijinga kama ya kwako na kuwa kwenye lindi la umasikini miaka nenda rudi.
Watoto wakusaidie, wewe baba ulikuwa wapi kutafuta mali? Kuwa mzazi siyo cheo hata paka anazaa pia
Kama unafikiri kuwa mzazi ni cheo halafu unasubiri watoto wako wakuhudumie, utakuja kuwalaumu sana wanao hawakuhudumii wakati wewe umeshindwa kutengeneza maisha bora kwako.
Elimu yenyewe umewasomesha kayumba, nyumba uliyonayo haieleweki halafu unasubiri wakuhudumie. Maisha yamebadilika sana kwa sasa
 
Na wale wakubwa zako wanakuja vizuri na watoto wao kumtembelea mzee au wamekausha?
 
Na wale wakubwa zako wanakuja vizuri na watoto wao kumtembelea mzee au wamekausha?
 
Kichwa Hakijakusaidia Chochote Zaidi Ya Kuwa Fenicha Kwenye Maisha Yako.
Kuanzia Leo Ukiulizwa Unamiliki Fenicha Ngapi Usisahau Kutaja Na Kichwa Chako.

Mtazamo Wa Kuona Mwafrika Na Uafrika Hauna Maana Ndo Umepelekea Tamaduni Za Kizungu Kutake over Hadi Nantumbo Ndani ndani Huko Kwa Mtazamo Wako Tegemea Siku Moja Wewe Au Mwanao Wa Kiume Kuletewa Mahari Ili Aolewe Na Kidume Mwenzake
Malezi Yanatakiwa Yawe Yale Yale Toka Babu Mzaa Babu Mpaka kwa Vitukuu Vya Vitukuu Vyako Ila Kwa Watu Kama Wewe Tegemea Majanga Zaidi Itafikia Wakati Hata Mtoto Wako Hutoweza Kumkalipia Na Ukifanya Hivyo Jela Inakuwinda.

Sikia Wewe Ukisikia Haki Za Wanawake Waasisi Ni Wanaume
Haki Za Mashoga Waanzilishi Ni Wanaume.
Cha Kukusaidia Nataka Ujitoe Huo Upande.
 
Kuna Mawili:Umri Wako Na Malezi Ya Upande Mmoja Yamechangia Ama Akili Zimechukua Likizo Bila Ruhusa (AWOL)
 
Huyu mzee Ana miaka 92 na ana watoto wameajiriwa huko serikalini Ila anauza samaki na kulalia mkeka

This is bullshit.

View attachment 3237690
Ha ha ha Mukululu
Huamini kuna watu wanaeza fanya hizo mambo leo hii ya 22nd century?

Kwanza kabisa nimecheka sana, muzee ya batu analala kwa mukeka, ikanikumbusha usemi ya mzungu "Sleep tight"

Hapo unakuta Muzee kulala chini ni kqamba kajipanga kikamilifu au sio? Labda hio ndio version yake ya Sleep tight๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

If he is comfortable and happy, what is the problem? Mnafikiri huyo mzee hajui the difference ya kulala chini na kulala kwenye godoro? Bulshit how?

Ana miaka 92 na anauza samaki, kuuza samaki ni jambo baya?

Hapana.

Nonetheless, Inawezekana kabisa kuwa muzee anavua, anakula na anauza samaki?

Kama anavua ina maana mzee bado ana nguvu zake na katika tamaduni nyingi duniani ni kitu cha kawaida kuona na kuwaachia wazee kuchapa kazi mpaka mauti. Enda Japan ujionee. Hakuna kulala mtu huko, especially kwa wazee.

Pia, Mzee kama asilimia kubwa ya diet yake ni samaki apewe maua yake. Bora samaki kuliko Pizza au Baga. Samaki na virutubisho vyake vnahusishwa na kuishi kwa binadamu kwa mda mrefu. Mzee ana 92apewe๐ŸŒน๐ŸŒน Ukimpeleka huyo muzee kwenye aging center kama zile za Ulaya na Marekani atakufa wiki mbili tu za kufika huko๐Ÿ˜…๐Ÿ˜

Sasa kama mzee anauza samaki unafikiri ni kwa nn asinunue Godoro mpaka wanae ndio wafanye hivyo?. Kama ana uza tafsiri yake ni kuwa mzee hana tatizo na hela kutoka kwa wanae. Vivyo hivyo na wanae kutokutilia mashaka na maamuzi ya mzee wao ni ishara wana imani na tamaduni zao, ama sio batanzani?
#######
In summary,comparisons zilizofanywa hapa na maudhui ya mada ndizo zenye dosari.
#######

Tumuonee huruma Mzee? Mmeanzisha michango ya kumnunulia godoro? Hapana

Tuwakemee wanae kwa kumtelekeza mzee wao? Je, walimemtelekeza kwa makusudi kabisa? Ama walimuachia Mzee afanye Maamuzi yake na kuyaheshimu?

Binafsi naamini mambo mengi yafanyikayo duniani humu yana baraka zote kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ikiwa na pamoja na moral and ethical values za jamii zote. Tuheshimiane tu


#culturalwar
 
Ila kuna wazee wengine wanashindwa kutengeneza maisha yao kuwa mazuri kwa sababu ya kuwatengenezea wtt wao maisha mazuri.
Km mzee wa umri huo anauza samaki ili ajikimu basi anaonekana ni mpambanaji. Km angekuwa mzee wa ovyo si hasha angekuwa hata ombaomba. Lkn anajua kazi ni utu na bado anatumika
 
Wazungu wanasema maisha yanaanza unapofikisha miaka 60. Umejiandaaje na uzee wako au unasubiri watoto wako wakuhudumie uzeeni?
Wazazi wengi wanashindwa kuishi na familia zao vizuri na kushindwa kutengeneza maisha ya uzeeni. Kama uliishi na familia yako kwa upendo na kutengeneza mazingira mazuri kwa watoto wako. Basi watakusitiri uzeeni ila usitegemee sana kwasasa kwasababu sasa hivi hela nidyo namba moja. Hapo ulipo unaishi kwa hela na mazingira ya kupata hela kwasasa yanazidi kuwa magumu.
 
Unakuwa mpambanaji halafu uzeeni unalala kwenye mkeka๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€ huyo mzee alikuwa anapambana na nn kwenye ujana wake?
 
Nazan maisha yake ya uanagika yamefanya aish miaka yote , japo ni vyema kuyaboresha ,

Wew unawez kuona anatesa lakn kwake its well and good , sometimes wazee hawa nivigumu kuwabadli na lifestyle yao.
 
Wahenga walisemaga hiv. "Ndani ya nyumba kuna kishindo kikuu."
Huwezi kujua chimbuko au sababu hasa ya kinachoendelea huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ