Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,662
- 6,888
Inaonekana kuwa kwenye Misa Takatifu huko kwenye Parokia ya Matosa, waume wamelazimishwa na Padri kuwaomba msamaha wake zao kwa namna ya 'udhalilishaji'. Nasema wamelazimishwa, kwani sidhani kama walikuwa radhi kufanya hivyo mbele ya watu.
Na ni 'udhalilishaji' kwa sababu jambo limefanyika hadharani na kupelekea baadhi ya waamini kuwacheka wanaume hao.
Pia, inaonekana pia baadhi ya wake zao hawakuwa tayari kufanyiwa hivyo, ila ndio hivyo kasisi kalazimisha. Pia, kwenye taratibu za Misa Takatifu, hakuna sehemu tendo hilo linafanyika!
Padri kafanya hivyo baada ya kupokea malalamiko ya baadhi ya wake juu ya waume zao. Lakini je, ndio ufanye kuwa ni matatizo ya wote? Kwa nini hakuwahita wahusika na kuwapa ushauri nasaha?
Nilifikiri, baada ya wanaume kuomba msamaha, wanawake nao wangefanya hivyo kwa waume zao!!! Najiuliza, hivi hao wanawake wamekuwa 'malaika'?
Je, ungekuwa ni wewe ungekubali kufanya hivyo kwa mkeo au kufanyiwa hivyo na mumeo?
View: https://youtu.be/cZwpZfGmR6Q?si=MBDiMUmOzyng9yiN