Hivi University Corner wako wapi?

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Hapa ninasikiliza interview ya Dr. Abbas msemaji mkuu wa serikali XXL, kwenye play list yake kachagua goma la Tshirt na Jeans, nikakumbuka hawa jamaa wa University Corner. Baada ya kutoa album yao iliyokuwa na vibao vikali wakapotea.

Tofauti na makundi mengine ambayo wasanii wake walau tunajua waliko hawa sijawahi wasikia kokote.
 
¶....Kiila mmoja anapendezaa....tishet na jinsi, hakuna inayomchukizaa tishet na jinsi, sintoweza kuiacha inanitoa chicha nami nawakilishaaa Tishet na jinsi........¶
 
¶....Kiila mmoja anapendezaa....tishet na jinsi, hakuna inayomchukizaa tishet na jinsi, sintoweza kuiacha inanitoa chicha nami nawakilishaaa Tishet na jinsi........¶
Enzi zetu hizo mzee,
Sahiv uzee ushagonga hodi 👵
 
Enzi zetu hizo mzee,
Sahiv uzee ushagonga hodi 👵
Kuna ile inaitwa sina nauli

Nataka kwenda kazini (sina nauli)
Nataka hospitalini (sina nauli)
Sina nauli sina nauli kabisa
Ndiyo maana ndugu tunashindwa kuonana

Long gone are the days when apple and blackberry were fruits.
Sasa hivi ni mwendo wa inama nichomeke, sijui ifinyie kwa ndani...
 
Kuna jinsi za buku wale wenzangu na Mimi,pita pita tandale t-shirt mpaka shilingi hamsini
 
Wewe mwenyewe hushangai,jeans wameivaa ulaya lakini ikiletwa bongo inaonekana inadai
 
"Jinsi haipigwi pasi wala jinsi haifuliwi, angalia sana jinsi nyeusi haipigwi kiwi"
 
Haaaaa Haaaaa 😂, Mara paka mate iteleze kama nyoka pangoni
 
Haaaaa Haaaaa 😂, Mara paka mate iteleze kama nyoka pangoni
Hatari tupu kuna nyimbo zikipigwa nikiwa na watu ninaowaheshimu najikuta eti niko busy na simu sijui kinachoendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…