⛽Hivi Ushawahi kuazima gari au umenunua gari halafu hujui pa kuwekea mafuta [fuel tank cap] ni upande gani?

⛽Hivi Ushawahi kuazima gari au umenunua gari halafu hujui pa kuwekea mafuta [fuel tank cap] ni upande gani?

Samatime Magari

Senior Member
Joined
Feb 10, 2017
Posts
119
Reaction score
457
1662995828501.png

Yani unaingia kituoni unapark gari uwekewe mafuta unajikuta umegeuza pump iko kulia wewe umeweka gari kushoto, Fuel attendant anakuona kama dish lako linayumba hivi hafu hakuelewi elewi.
.
Kuna wale wasee huwa hawataki aibu ndogo ndogo huwa wanashuka wanachungulia kwanza, Yani kabla hajafika kituoni anashuka anaangalia upande wa tank ndo anaingia kituoni..
.
Sasa naenda kukupa mbinu itakayokusaidia kujua upande wa tank [fuel tank cap] bila kushuka kwenye gari, Kujua upande wa kuwekea mafuta [fuel tank cap] angalia kwenye gauge ya mafuta kwa dashboard utaona ki mshare kiko hapo..
.
1662996635143.png
1662996702171.png

.
Hicho kimshare kikiwa kina point kushoto basi jua kwamba upande wa kuwekea mafuta ni kushoto na kikiwa kinapoint kulia basi pa kuwekea mafuta ni kulia..
.
Nakuongezea na bonus tips 4 kuhusu mfuniko wa mafuta ambazo wengi hawazijui na utazijua ndani ya dakika 1 tu, Ukifungua mfuniko wa nje wa Tank kuna kishimo kiko pale kwa ajili ya kutoa maji [drainage] sio gari zote.. . Hiki huwa kinaziba maji yanatuama yanatengeneza unyevu..
.
Unyevu unaleta kutu inashika kwenye bawaba za mfuniko mwisho wa siku mfuniko wa nje unakatika, So kikiziba tafuta spoke au wire chokonoa ikawe sawa ili maji yakiingia yatoke..
.
Hii itakusaidia usije ingia gharama ya kununua mfuniko mpya maana hakuna bawaba za vimfuniko, Halafu incase mfuniko wa nje wa tank la mafuta umekata/umegoma kufunguka..
.
1662996781784.png
1662996797776.png

.
Angalia kwa ndani upande wa pili utaona space ukipachua utakua ki handle cha kuvuta kufungua manually.. . Kuna baadhi ya gari bawaba zinaonekana so kama zimepauka paka hata mafuta ya nazi ziwe laini..
.
Hivi nimesema nakupa tips nne ehee, mbili tayari twende ya tatu, Kama umeazima gari na haujui inatumia Petrol au Diesel angalia mfuniko wa nje kwa ndani kuna sticker inayoonyesha mafuta gari inayotumia..
.
Kama hamna sticker mpigie mwenye gari muulize tu hapo pamoto kidogo usilete ujuaji utaleta shida, habari za kushusha tank kufanya flushing na usafi ni ndefu kidogo..
.
1662996954205.png
1662996976758.png


.
Mwisho ukiwa unaweka mafuta yule pump attendant akifungua mfuniko wa ndani, Kama una ki kamba/hook asiuache uniinginie unakuaga na mafuta kidogo na yakigusa body inawahi kupauka/corrode.
.
Kuna sehemu maalumu ya kupachika huo mfuniko wa ndani wakati unaweka mafuta, Kama hauna hook asiuweke juu ya body la gari. ukiweka pale juu unamwaga mafuta then yanasambaa yanachangia kupauka kwa gari juu..
.
1662997272412.png
1662997290566.png

.
Kwa tips zaidi kuhusu magari endelea kufatilia kurasa zetu za jamii ili next time usipitwe na tips kama hizi, Kwa wenye issue yoyote kuhusu magari [ ushauri, kuagiza, kununua, kutengeneza nk ]
.
Pia unaweza kututembea ofisini Posta Mpya Phoenix house ilipokua NMB zamani Dar es salaam mkabala na Benjamini Mkapa Tower kwa maelezo zaidi.. Sharing is caring sasa kama umejifunza kitu usisahau kushare na wadau wa magari wapate madini pia kama ulivyopata wewe..
.
Asante
Samatime Car Dealers Co Ltd
0714547598
 
Back
Top Bottom