SoC01 Hivi ushawahi kujiuliza chanzo cha picha za utupu ni nini?

SoC01 Hivi ushawahi kujiuliza chanzo cha picha za utupu ni nini?

Stories of Change - 2021 Competition

Ornate

Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
26
Reaction score
33
Hivi ushawahi kujiuliza chanzo cha picha za utupu ni nini? Ama chanzo kuvujishwa kwa siri za wakati wa tendo la faragha ni nini?

Imekuwa janga kubwa kwa Taifa, ingawa inaonekana kupendwa na vijana wengi wa Tanzania, sijui niite nini, maana nikisema ni ushamba haitoshi kuelezea hili, itoshe kusema ni ushamba uliokithiri. Wanaonekana kuathirika na mitandao ya kijamii huku ikiwa ni moja ya sababu za uvivu na kudumaza akili isifikirie mambo ya msingi.

Kwa kujua na wengine bila hata kuelewa, vijana wamejikuta katika matatizo makubwa ya kupoteza utu wao hasa wasichana, mara nyingi wanajipiga picha za utupu na kutuma katika mitandao ya kijamii bila kujua kuwa wanajidhulumu kingono.

Inasikitisha kuona mtu aliyekuwa faragha na mpenzi wake na anadiriki kutuma au kuvujisha ufaragha wake katika mitandao ya kijamii

Ni ukweli kwamba vijana ni nguvu kazi ya Taifa, lakini sasa giza limetanda, hawaoni mbele, mitandao ya kijamii imekuwa Mungu kwa vijana wengi, hakuna tena muda wa kuleta maendeleo, wameishia kukesha mitandaoni na kuangalia mambo ya aibu huku wengine wakijisahau kabisa na kujikuta wanatuma vitu visivyostaili, eti wanaiga maisha ya wasanii,na fikra zilizojaa akilini mwao kwamba ni maendeleo ya sayansi na tekinolojia.

Ndio, ni maendeleo lakini, emu jiulize kama ukitumia mitandao ya kijamii, kutangaza biashara mbalimbali ina faida kiasi gani? Na kutuma picha za utupu pamoja na kukesha kufuatilia maisha ya wasanii Kuna faida gani?

Tenga muda tafakari athari zake ni nyingi mno, sio kwa taifa tu lakini hata kwa mmoja mmoja ikiwa ni pamoja na wimbi kubwa la umasikini kwa vijana kutokana na kukosa muda wa kufikiri na kubuni njia mbalimbali za kujiingizia kipato, kwa kuilewesha akili kutazama mambo yasiyo na msingi " inang'ata"

Amka, tafuta mbinu mbalimbali zitakazokuwezesha kufikia malengo yako kupitia mitandao ya kijamii, ndio, yapo mengi ya kufanya tangaza biashara yako kupitia mitandao hiyo, tengeneza blogu zitakazokuongezea watazamaji na kujipatia kipato.

Chukua hatua tafakari, ,inang'ata' inapotumiwa vibaya huku 'inapuliza' kwa kukusahaulisha ili usiachane nayo.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom