Hivi Virusi vya UKIMWI vinaonesha Idadi ya wadudu waliopo mwilini?

Hivi Virusi vya UKIMWI vinaonesha Idadi ya wadudu waliopo mwilini?

Niache Nteseke

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2020
Posts
2,162
Reaction score
2,616
Habari zenu wakuu.

Natumai mnaendelea vyema kabisa. Well, swali langu ni kutaka kufahamu mtu anapoenda kupima Virusi vya UKIMWI, huwa vinaonesha Idadi ya wadudu waliopo ndani ya mwili wakuu?

Na je, Idadi hiyo ikiwa kiasi gani ndio huwa na madhara zaidi kwa mwili na katika kupungua Idadi ya vijidudu hivyo huwa inaweza kupungua mpaka kufikia ngapi?

Natanguliza shukran. Thanks.
 
Kinachopimwa ni antibodies (reaction) ya virus na kinga ya mwili.

Ukipima kawaida yani kujuwa afya huwa haionyeshi idadi ni kama kipimo cha mimba tu.

Ukiwa na maambukizi ukaanza kutumia dawa huwa wanapima Viral load yaani kiwango cha virus nadhani hapa ndo kuna jibu lako!

Unakuta machine inasoma 1000 copies it means huyu mtu ana virus 1000 but kitaalam sio kwanba kweli ni hiyo idadi bali ni kiashiria kuwa CD4 zako zimeshuka ndo maana reaction ya virus iko juu.

Lakini ukikuta 0 copies hadi 20 maana ake CD4 (Kinga ya mwili) iko juu (Target Not Detected) huyu mtu hawezi nyemelewa na magonjwa.

Tafsiri yake anatumia dawa vizuri.
 
Kinachopimwa ni antibodies (reaction) ya virus na kinga ya mwili.

Ukipima kawaida yani kujuwa afya huwa haionyeshi idadi ni kama kipimo cha mimba tu...

Oooh Owkay nimekupata vyema kiongozi, ina maana unapokuwa na 0 copies na ukaendelea kutumia dawa hii tafsiri yake ni ipi, ni kuwa unakuwa hauna virusi kabisa au inakuaje mkuu...?

Na mtu kama huyu akifanya mapenzi na mtu ambaye -ve ataweza kumuambukiza virusi ilhali ni 0 copies kiongozi?

Na je, anapoacha kutumia dawa hali itakuaje, vidudu vitarudi tena na kuongezeka au inakuaje hapo?

Na katika kiwango gani hali ya mgonjwa inaweza kuwa mbaya kwa Idadi ya vijidudu, yaani vikifika idadi gani mgonjwa anaweza akapata maradhi na kuanza kuumwa?

Na katika hiyo 0 copies akipima HIV anatambulika kama +ve au anatambulika ni -ve...? Na akipima atajulikana kuwa ni muathirika ilhali ana zero copies?

Msaada katika hilo mkuu. Thanks.
 
Habari zenu wakuu.

Natumai mnaendelea vyema kabisa. Well, swali langu ni kutaka kufahamu mtu anapoenda kupima Virusi vya UKIMWI, huwa vinaonesha Idadi ya wadudu waliopo ndani ya mwili wakuu?

Na je, Idadi hiyo ikiwa kiasi gani ndio huwa na madhara zaidi kwa mwili na katika kupungua Idadi ya vijidudu hivyo huwa inaweza kupungua mpaka kufikia ngapi?

Natanguliza shukran. Thanks.
Huwa wanapima athari za vidudu. siyo vidudu vyenyewe. Hawavioni hivyo.
 
Oooh Owkay nimekupata vyema kiongozi, ina maana unapokuwa na 0 copies na ukaendelea kutumia dawa hii tafsiri yake ni ipi, ni kuwa unakuwa hauna virusi kabisa au inakuaje mkuu...?

Na mtu kama huyu akifanya mapenzi na mtu ambaye -ve ataweza kumuambukiza virusi ilhali ni 0 copies kiongozi...

1--Virusi unakua navyo , isipokua Kiwango chake katika damuni kipo chini kiasi kwamba ningumu kugundulika kwa vipimo vya kawaida vinavyotizama antigen wa HIV .

2-copies chini ya 20 kwa kila mililita ya damu hawez kuambukiza mtu kwa ngono.

3-Ukitaka Kukata kamba mapema Acha kutumia Dawa sababu Copies ziko below 20, watarudi kwa nguvu ya kustaajabisha ( ndio sababu waliaoanza kisha wakaacha hufa mapema).

4--copies kuanzia laki moja ni kiwango kibaya sana, kuna wengine unakuta anampaka milion moja nausheeeee , hususani kwenye miezi mitatu ya kwanza ya maambukizi kunakua navirusi wengi sanaaaaa . Heri ukutane na mwenye virusi wa mwaka mmoja, kuliko kukutana na mwenye virusi wa mwezi mmoja hadi mitatu ya maambukizi.

5-Ukishapata HIV hata km viral load itasoma below 20 copies yaan undetectable , Ukipima HIV rapid test Itasoma tu positive ..kwa ufupi, kinga ya mwili huzalisha antibodies specific kupambana na HIV, mtu anapopata mamabukizi, hizi antibodies hubakia maishani mwake kote mpaka anapokata kamba, kwaiyo hata atumie Dawa vipi, Rapid tests zitasoma tu .

Utumiaji sahihi wa ARVs , Hupunguza kiwango cha virusi, Kinga itaimarika, huwezi pata magonjwa nyemelezi na mtu huishi maisha marefu sawa na asoumwa na yenye furaha na kutimiza ndoto zake.
 
Back
Top Bottom