Oooh Owkay nimekupata vyema kiongozi, ina maana unapokuwa na 0 copies na ukaendelea kutumia dawa hii tafsiri yake ni ipi, ni kuwa unakuwa hauna virusi kabisa au inakuaje mkuu...?
Na mtu kama huyu akifanya mapenzi na mtu ambaye -ve ataweza kumuambukiza virusi ilhali ni 0 copies kiongozi...
1--Virusi unakua navyo , isipokua Kiwango chake katika damuni kipo chini kiasi kwamba ningumu kugundulika kwa vipimo vya kawaida vinavyotizama antigen wa HIV .
2-copies chini ya 20 kwa kila mililita ya damu hawez kuambukiza mtu kwa ngono.
3-Ukitaka Kukata kamba mapema Acha kutumia Dawa sababu Copies ziko below 20, watarudi kwa nguvu ya kustaajabisha ( ndio sababu waliaoanza kisha wakaacha hufa mapema).
4--copies kuanzia laki moja ni kiwango kibaya sana, kuna wengine unakuta anampaka milion moja nausheeeee , hususani kwenye miezi mitatu ya kwanza ya maambukizi kunakua navirusi wengi sanaaaaa . Heri ukutane na mwenye virusi wa mwaka mmoja, kuliko kukutana na mwenye virusi wa mwezi mmoja hadi mitatu ya maambukizi.
5-Ukishapata HIV hata km viral load itasoma below 20 copies yaan undetectable , Ukipima HIV rapid test Itasoma tu positive ..kwa ufupi, kinga ya mwili huzalisha antibodies specific kupambana na HIV, mtu anapopata mamabukizi, hizi antibodies hubakia maishani mwake kote mpaka anapokata kamba, kwaiyo hata atumie Dawa vipi, Rapid tests zitasoma tu .
Utumiaji sahihi wa ARVs , Hupunguza kiwango cha virusi, Kinga itaimarika, huwezi pata magonjwa nyemelezi na mtu huishi maisha marefu sawa na asoumwa na yenye furaha na kutimiza ndoto zake.