Hivi wachezaji wa timu za ulaya wakiwa majeruhi wanaruhusiwa kwenda kwao kutatua matatizo ya kifamilia?

Hivi wachezaji wa timu za ulaya wakiwa majeruhi wanaruhusiwa kwenda kwao kutatua matatizo ya kifamilia?

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
de3e0fd56e2216459ae008f4aad1f822.jpg
e600987adb62b456f84897540819b46e.jpg
Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Sports Club, Masoud Djuma amenukuliwa kwenye gazeti moja la michezo, amesema kuwa endapo atashindwa kurekebisha nidhamu ya staa wa Simba SC Emmanuel Okwi, atasepa na kurejea kwao huku akiuambia uongozi wa Simba kuwa amamtaka Okwi arejea haraka na kuungana na timu Zanzibar.

Naunga mkono kauli hii asilimia 100% maana upuuzi huu umetamalaki sana hasa timu hizi mbili za Simba SC na Yanga FC, na kwanini viongozi wanakuwa wazito kushughulikia suala hili la utovu wa nidhamu au kuna namna fulani kati ya kiongozi au mchezaji?

Kwa kweli tabia ya mchezaji kupata jeraha la enka kidogo safari kwao naiona hapa nchini tu. Hivi wachezaji wa timu za ulaya wakiwa majeruhi wanaruhusiwa kirahisi kweli kwenda kwao kutatua matatizo yao ya kifamilia? Cha ajabu hata akipona bado harudi kwa wakati.

Na kama kocha anaponda utaratibu huu, je sisi mashabiki na wanachama tusemeje? Ni vema kuponda huu ujinga wa ruhusa kwa wachezaji wa kigeni kurudi kwao kwa matatizo ambayo hakuna ulazima wa kufanya hivyo.

Ligi ya VPL na Michuano ya Mapinduzi na FA ni michache sana kwa mchezaji kuitumikia klabu ambayo inamlipa fedha nyingi sana, lakini cha kushangaza Simba SC na Yanga FC ndo wako mbele kubariki utaratibu huu wa ruhusa kwa wachezaji mpaka wengine kuamua kulima na kupalilia shamba huko kwao Zambia.

Ni wakati sasa wakung'amu hili ambalo limeota mizizi, ninyi viongozi wa Simba SC na Yanga FC kuweka adhabu kali sana kukomesha ujinga huu wa mchezaji kula mshahara wa bure huku yuko kwao halafu timu ikivurunda kocha ndo mchawi.
 
Si kama wafanyavyo Simba na Yanga, viongozi wanawaogopa mno wachezaji wa kigeni
Ni kweli mkuu simba na yanga mchezaji akicheza mechi Tatu utamsikia kaenda kwao Rwanda au Uganda.ubabaishaji ni mwingi mchezaji anakuwa juu ya klabu.ulaya huu ujinga haupo.mfano wanyama anaumwa miez miwili sasa but hajarud Kenya yupo england mana anahudumiwa kila kitu na klabu yake.hapa kwetu kila siku niyonzima na okwi wapo kwao na hawaambiwi kitu.namuonea huruma sana irambona maana hana full authority ya kuwaadhibu wachezaji.utumbo mwingine Manula yupo kwenye maandaliz ya kufunga ndoa kipindi hiki kwahiyo hayupo kwenye timu.ulaya ndoa nyingi wanafunga mwishoni mwa msimu
 
Si kama wafanyavyo Simba na Yanga, viongozi wanawaogopa mno wachezaji wa kigeni
Sio kwamba wanawaogopa, isipokuwa wanagawana mshahara na vigogo hata pesa za usajili.

Mchezaji anasajiliwa kwa milioni 50 kumbe ya kwake 25 tu ..... wanatangaza mshahara mil 5 kumbe ya kwake 2.5 tu..

Na hao ndio wanaompa kiburi mchezaji.
 
Aisee mkuu itakuwa kweli ndo mana wajomba wanajiamulia watakavyo.mfano okwi ruhusa iliisha jumanne ad Leo hajarudi
 
Sio kwamba wanawaogopa, isipokuwa wanagawana mshahara na vigogo hata pesa za usajili.

Mchezaji anasajiliwa kwa milioni 50 kumbe ya kwake 25 tu ..... wanatangaza mshahara mil 5 kumbe ya kwake 2.5 tu..

Na hao ndio wanaompa kiburi mchezaji.
Ndo maana kwenye thread hapo nimeuliza au kuna namna kati ya kiongozi na mchezaji? Haiwezekani mchezaji awe juu kuliko klabu bhana
 
Silva aliomba ruhusa ya kwenda hospitality ambapo mkewe alijifungua mtoto njiti hivyo alienda kutoa support kwa mama na mtoto
Asante mkuu kwa unyambulifu na ufafanuzi. Nililishwa tango pori hapa. Ingekuwa ajabu sana ulaya kuwa na ujinga wa namna hii
 
Asante mkuu kwa unyambulifu na ufafanuzi. Nililishwa tango pori hapa. Ingekuwa ajabu sana ulaya kuwa na ujinga wa namna hii
Poa mkuu.ulaya wapo serious sana kwa matatizo nyeti hukatazwi kwenda.guardiola kampa Silva Uhuru anaruhusiw kwenda mda wowote na kurud mda wowote had halo atakapoona mambo yamekaa saw a.ukiingia web ya man city utaikuta hiyo habar kwa undani
 
Sio kwamba wanawaogopa, isipokuwa wanagawana mshahara na vigogo hata pesa za usajili.

Mchezaji anasajiliwa kwa milioni 50 kumbe ya kwake 25 tu ..... wanatangaza mshahara mil 5 kumbe ya kwake 2.5 tu..

Na hao ndio wanaompa kiburi mchezaji.

Cc: Shariff "Casillas"
 
Km unahisi ni kutatua matatizo ya kifamilia ya baba na mama,shtuka mkuu,hao wanaendaga kuroga
 
Sio kwamba wanawaogopa, isipokuwa wanagawana mshahara na vigogo hata pesa za usajili.

Mchezaji anasajiliwa kwa milioni 50 kumbe ya kwake 25 tu ..... wanatangaza mshahara mil 5 kumbe ya kwake 2.5 tu..

Na hao ndio wanaompa kiburi mchezaji.
Leo tuonane la stanza nikupe kinywaji unachokunywa
 
Back
Top Bottom