Hivi Wachezaji wetu wanaocheza nje ya nchi hawajajiongeza kutusaidia mapambano dhidi ya Corona?

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Salaam.

Serikali yetu imetualika wote tuisaidie michango dhidi ya huu ugonjwa, baadhi wameshajitolea kuonesha mfano akiwemo Ndugu Rostam Aziz alietoa vifaa kukabiliana na huu ugonjwa, na kiasi kilichopatikana kinakaribia kufika Tsh. bil 6.

Waswahili husema kutoa ni moyo na sio utajiri, najiuliza hawa wachezaji wetu wanaocheza nje ya nchi bado mpaka leo hawajashtuka nao wachangie chochote?

Maana nawaona wako "busy" tu kutuonesha walivyojifungia ndani kuogopa kupata maambukizi, au hawana watu proffesional wakuwashauri kuhusu nini wafanye na kipi wasifanye, japo kwa hili sidhani kama panahitajika mtu akumbushwe maana sote tunaona Corona inavyotukimbiza kwasasa ulimwenguni.

Sasa inakuwaje hawa jamaa zetu nje ya nchi wamepasahau nyumbani!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
duuh misaada, misaada, misaada. tunaamini katika ombaomba. lakini usimwangalie messi/ ronado/mane/salah wanavyotoa misaada ukataka na hawa wa kwetu watoe hivyohivyo, wanapishana parefu sana kimapato
 
Wako wangapi hao wachezaji? pili pana namna mbili za kutoa kimya kimya au kutangaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…