Hawa jamaa ndio wanaosimamia maduka ya dawa maarufu kama Pharmacy.
Jana nimeona wameungana na wanaharakati akina shangazi, kupinga agizo la mheshimiwa waziri Ummy, la kuondoa maduka ya dawa yaliyo karibu na Hospitali za umma kama inavyosema sheria yao wenyewe.
Sheria au kanuni ziliweka umbali wa maduka ya dawa na Hospitali,lakini pia umbali wa pharmacy na pharmacy bila kusahau umbali wa pharmacy na duka la dawa muhimu.
Lengo la sheria hizi lilikuwa kupeana nafasi za kufanya biashara. Kila mmoja mwenye pharmacy apate wateja.Pia lengo lilikuwa kuhakikisha huduma hii inasambaa sehemu nyingi ili kuwakaribia wananchi.
Sheria hii walitunga wao wenyewe,kupitia kwenye baraza lao wenyewe, na waliipitisha wao wenyewe kwa manufaa yao wenyewe kwani ililenga kulinda maslahi yao wenyewe.
Mfano ni pale wanapokataza duka la dawa muhimu lisiwepo mjini. Na waliwahi kujaribu kuyaondoa yote hata yaliyokuwepo tangu enzi za Mwinyi ili hawa wanaofungua sasa hivi wapate nafasi.
Kimsingi sheria hii haikuwa na umuhimu wowote pamoja na sababu walizozitoa.
Duka la dawa ni biashara, pamoja na kuwa ni huduma pia,wamiliki wana haki ya kuchagua eneo ambalo kwao wanadhani wataweza kufanya biashara hiyo kwa uzuri zaidi ili mradi wanazingatia sheria.
Leo ninawashangaa sana kwa kumgeuka waziri kana kwamba, amejitungia mwenyewe hizo sheria.
Wanajiweka kwenye kundi la watu wanaoonewa na wanasiasa, wakati sheria wametengeneza wao wenyewe. Huu si uungwana kabisa.
Mkilaumu, mlaumu baraza lenu la wafamasia, ambao kwa upande mwingine, wamekuwa wakilinda sasa maslahi yenu hata mnapovunja sheria,na siyo kumlaumu Ummy.
Kumbukeni ni huyu huyu Ummy, alitoa maagizo, wauguzi wote waondolewe pharmacy,ili wafamasia watumike katika kazi zao.
Alipokuja Gwajima, akasema ninyi ni wezi, hamuaminiki, hivyo akaendelea kuwa na wauguzi na wahudumu wa afya kwenye pharmacy za serikali. Hata ajira hakutoa za kutosha, licha ya vituo vya afya kuongezeka mara dufu. Huyo Gwajima ndiyo alikuwa rafiki yenu.
Mjisahihishe kwa kutumia akili zenu vizuri kumshauri waziri, na siyo kumpotosha hadi mnatunga sheria, halafu mnakuja kumgeuka