Hivi Waganda wana tatizo gani?

Labda hawaijui jamiiforums, labda ningekuuliza wewe upo kwenye forums zu Waganda ukichangia?
Kule taarifa za habari nyingi kilugha hata na sio English utapost wapi. Mr Nice alipiga sana mpunga kule kiswahili wanakifuatilia.
 
Mimi kwa maoni yangu ni bora hata wangeweka Forum ya Rwanda/Burundi kuliko Uganda, kwani habari za Rwanda/Burundi hata ni nyingi zaidi klk za Uganda, Warundi/Nyarwanda TZ in wengi zaidi kuliko Waganda.
Forum ya Rwanda itakuwa ya moto kwa mabinti wa kule wana mvuto mi naona ianzishwe leo leo wazo safi sana naunga mkono
 
Kila mtu huchangia humu kwa mtazamo wake, hivyo isikupe stress, ila kusema Waganda wana aibu utakua unadanganya, wao hujimix sana na wana ujasiri, sio kama nyie waoga waoga, Mtanzania akiwa nje ya nchi ni mwoga sana.

Huo ni uongo uliopitiliza, uzuri nimekaa na waganda ndani ya Tanzania, Uganda kwenyewe na nje ya Afrika. They are among the humble Afrikans.

Wee ni lini ulikutana na mTanzania nje ya Tanzania akawa muoga??

Usiniambie kwamba walikataa kukwapua ndiyo ikawa kipimo chako cha uoga. Maana nyie neno aggressive mnalitumia tofauti. Nyie kwenu kuiba ndiyo aggressiveness.
 
Forum ya Rwanda itakuwa ya moto kwa mabinti wa kule wana mvuto mi naona ianzishwe leo leo wazo safi sana naunga mkono
Tatizo mabinti wao wanafanana uzuri tofauti na tz wametofautiana uzuri yaani tz uzuri tofauti tofauti
 
Forum ya Rwanda itakuwa ya moto kwa mabinti wa kule wana mvuto mi naona ianzishwe leo leo wazo safi sana naunga mkono
Tatizo mabinti wao wanafanana uzuri tofauti na tz wametofautiana uzuri yaani tz uzuri tofauti tofauti
 

Kaka nimefanya kazi na Waganda huko huko Tanzania, hivyo hamna jipya unaloniambia kuwahusu, wakiwa huko mara nyingi hupiga kimya maana hamuendani kwa vile nyie ni watu wa ze ze ze. Nakumbuka Mganda mmoja tukiwa naye huko alikua ananichangamkia na kuongea sana, ila akibaki na Wabongo utadhani yeye bubu, hili nimewahi kuliona hata kwa Mmarekani.

Watanzania ukiondoa Wachagga, wengine wote waoga waoga, nakumbuka Mtanzania mmoja tulimtuma Kenya kipindi hicho nikiwa Bongo, ni jamaa mmoja mtemi na mgomvi sana kwenye bar za Tanzania, ikatokea tunahitaji vipuri ambavyo vipo vinauzwa Nairobi, yaani niliangua kicheko pale jamaa aligoma hatalala Kenya kwamba anaogopa, aliomba kwa namna yote ahitimishe shughuli Kenya na kugeuza.

Kwa Watanzania, lada Wachagga na Wahaya ndio huwa nawaona huku wamechangamka, watu wa kujituma na kuchakarika, sio waoga waoga, Wachagga utawakuta hata Somalia kwa mabomu wanapiga mishe. Nyie wengine hamnazo.
 
Tatizo mabinti wao wanafanana uzuri tofauti na tz wametofautiana uzuri yaani tz uzuri tofauti tofauti
Madem wa Rwanda wamefanana fanana,
Uzuri wa Tanzania kuna madem wa kila aina 😂😂😂
 
Mkuu mbona unaenda nje ya mada,hapa tunazungumzia waganda wewe unaleta masifa ya wakenya...!
Kuna mmoja huko juu amesema waganda wanaringa na kujiona class sana, nikasema labda hawajui wakenya nini? Hivi ukanda huu kuna watu wanajiona cake kama wakenya?
 
Unajifanya kutujua sana huna lolote we mkeii
 
LOL yaani ni washamba na malimbukeni lakini wenyewe hata hawajishtukii

Hehehe na bado mtakoma ubishi, humu JF kuna Wakenya wasiozidi kumi ila utadhani tuko laki moja, yaani Mkenya ni balaa kupita maelezo, hadi raha.
Hebu nionyeshe wapi Watanzania mnasikika kwenye jukwaa la kijamii la kimataifa, ukienda Twitter tumegaragaraza huko, mpaka juzi Watanzania wamejitutumua kuiga KoT kwa kubuni ToT.
Kule Nairaland Wanigeria hawana hamu na Wakenya wanaotetemesha jukwaa lote, hata hawazidi watano.
 

BADO UNAWAJUA Waganda kwa sehemu ndogo sana. Pia kwa waTanzania unawajua kwa kiasi fulani, unaongelea experience ya kipindi cha Nyerere. Labda sijui kuchangamka una maanisha nini?
 
Ulimbukeni wenu ni kuvikumbatia vya mzungu na kuwatema mate waafrika wenzenu kisa ya uafrika wao

Kuhusu mitandaoni ni kwamba hujawajua tu watanzania, watanzania utawapata kwenye mambo ya burudani na ndio maana watanzania wanaongoza kuwa watu wenye furaha muda wote, hata ukiangalia huku namna wanavyochat utaona kutumia emoji za kucheka ni kawaida yao hata kwenye mambo ambayo hayahitaji kucheka

Ndivyo tulivyo ndivyo tulivyoumbwa, kwa hiyo huko twitter kwenye kuangushana mieleka na kujipatia ugonjwa wa kiharusi nani anataka? Watanzania wapo insta wanaenjoy maisha bila stress
 
Kuna uzi ulikua unapiga kelele kama alizo piga dada yako huddah kuwa wa Tz ni wauza unga wakubwa na majambazi uko SA. Leo umechange gear nakusema ni waoga!
 

Kwanza kabisa hakuna Mwafrika ambaye hajakumbatia kila kitu cha mzungu hadi unavyokunya na kula, unachovaa, kifaa unachotumia humu kuandika, herufi..yaani hadi basi, hivyo huna jeuri ya kumsema mwenzako anaayevitumia.
Kuhusu furaha, emoji emoji sio kiashiria cha furaha maana nyie nawajua mlivyo wanafiki, huwa mnacheka cheka lakini kiundani mumeyabeba majungu na machungu, hivi unafahamu Tanzania ni mojawapo wa mataifa kumi duniani ambayo raia wake wanaishi kwa dhiki.
Hebu waza, mumewekwa kwenye kundi moja na Syria ambao wanachezea mabomu kila siku, yaani itakua mna roho nyeusi kiasi cha kufa mtu, kwamba uwekwe kwenye kundi moja na watu wanaopigana ila wewe kwako unakenua meno hupigani.
Hehehe!! ila poleni ndugu zetu....

 
Kuna uzi ulikua unapiga kelele kama alizo piga dada yako huddah kuwa wa Tz ni wauza unga wakubwa na majambazi uko SA. Leo umechange gear nakusema ni waoga!

Kutumika kama shehena la kubeba madawa sio kiashiria cha ujasiri ila ni utumwa na ujinga, maana unapeleka hayo mavitu kwa Wachina ukijua watuhumiwa wananyongwa huko.
Hapa naongea kuhusu ujasiri wa kujimix kwenye ndani ya watu wasio wa nchi yako na kuchakarika na kufanya mishe kwa njia halali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…