GE2025 Hivi wagombea urais na ubunge wanatuonaje watanzania?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The lariat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2025
Posts
1,351
Reaction score
1,928
Hivi hawa watu wanagombea nafasi mbali mbali za kisiasa wanatuonaje.

Mmoja kasema akipata urais vijana wataruhusiwa kulima bhangi, mwingine kasema kila mtanzania atapewa simu janja na vocha bure, mwingine atamleta mcheza cinema maarufu Arusha, mwingine anasema vitanda vya sita kwa sita itakua marufuku ile mke na mume walale wamekumbatiana.

Hawa wa ubwabwa wanasema kilo ya Michele itakua sh 500 na ukifika hospitali unapewa sahani ya ubwabwa ushushie dawa. Mwingine atajenga bwawa la mamba ikulu lkn pia kuna yule aliyesema mtoto akizaliwa tu anapewa posho ya laki tano.

Mwingine ambaye yuko madarakani siku nyingi anasema akipewa ridhaa tu atajenga soko. Jamani soko linajengwa na halmashauri au central government?

HIZI DRAMA NAZIONA PEKE YANGU TU AU NA NINYI WENZANGU MNAZIONA?
 
Siwezi kwenda kwenye kampeni za kiongozi yoyote kama tu kuendesha mwendo kazi wameshidwa wanaweza kwenda kusikiliza nini hawana mawazo mapya ya kutatua changamoto za watu
 
Wamebaki na mbinu ya kuwasomba watu kwenye malori na kuwaleta mkutanoni, nachojiuliza hawa watu wakifika kusikiliza sera wanaambiwa watajengewa soko, mara anawaambia yeye sio wa wanyonge!!!
 
Siwezi kwenda kwenye kampeni za kiongozi yoyote kama tu kuendesha mwendo kazi wameshidwa wanaweza kwenda kusikiliza nini hawana mawazo mapya ya kutatua changamoto za watu
Wewe kiazi leo unasema hivi kesho unasema hivi Yuda Eskariote kabisa wewe hueleweki upo upande upi huku upo na huku upo stupid
 
Wewe kiazi leo unasema hivi kesho unasema hivi Yuda Eskariote kabisa wewe hueleweki upo upande upi huku upo na huku upo stupi

Wewe kiazi leo unasema hivi kesho unasema hivi Yuda Eskariote kabisa wewe hueleweki upo upande upi huku upo na huku upo stupid
Umenikosea sana mimi ni mtu huru mawazo yangu hayajafungwa na chama chochote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…