hivi wajua NYANYA na VIAZI ni SUMU?(chips)

Kufanya matusi na kula nyanya ipi bora?!

Mwisho mtatuambia tule nyanya zinazotokana na alovera kutoka forever living product ndo salama.
 

AND REMEMBER THAT HUMAN BODY IS THE LARGEST AND COMPLEX LABORATORY EVER. So it control most of the things dosed to it properly.
 
ni nyanya mbichi tu au pamoja na tomato sauce? loooh jamani chipusi na tomato sauce mbona balaaa.
 
maji ya bomba kwa watoto wa uswazi wala siyo sumu lakini kwa wale watoto wanaotumia maji ya chupa (mineral water) ni sumu tosha.
 
Hivi wale wavuvi wa baharini kwa nini hupiga piga pweza kwa fimbo si chini ya dakika kadhaa kabla ya kumpatia mteja kitoweo chake aende akakiandae nyumbani kwakwe au hotelini? hivi huwa wanatoa sumu kwenye minofu ya pweza? kwa hiyo pweza hawezi liwa mpaka atandikwe viboko?
 
In the long run we are all dead keep enjoying.. Hata vauchers wapo kwa sababu maalum...
 
Aise tumeshashoshwa na haya mambo, yaani siku hizi kila kitu ni sumu.
Mi kuna mtu alinichosha pia kwa kuniambia kunywa maji ya moto (hasa kwa wanopunguza mtumbo)eti maji ya moto yanasababisha kansa ya koo

Mbona mnatutisha sana. kila kitu ni sumu sasa... tule nini??????
 
Wanadamu tuko exposed kwenye kemikali mbali mbali kutokana na vyakula tunavyokula, hewa tunayovuta na mazingira yanayotuzunguka. Na mwili wa binadamu continously unapambana na hizi kemikali kama zina madhara kwa binadamu. Ni pale tu kemikali hizi zinapoingia kwa kiasi kikubwa mwilini au kukaa mpaka zikafikia hatua kuwa mwili unashindwa kuzishughulikia ndipo tunaona maradhi yanampata mwanadamu. Lakini kama walivyosema wakuu wengine, almost everything we eat or drink is potentially poisonous.
 
Mleta Uzi - Ukimchunguza Kuku hutamla! Usituharibie hamu ya kula, hembu nenda kaagize Chips halafu jamaa akukatie na Nyanya kwa pembeni na Mazagazaga mengine halafu sikilizia utamu wake.
 
Mleta Uzi - Ukimchunguza Kuku hutamla! Usituharibie hamu ya kula, hembu nenda kaagize Chips halafu jamaa akukatie na Nyanya kwa pembeni na Mazagazaga mengine halafu sikilizia utamu wake.

Aisee wakati Mwingine semi zetu husaidia pia.. Kama hoja Za wananchi humu .. Takriban kila kitu ni sumu, nimejaribu kuangalia baadhi ya vyakula nikagundua ukisoma sana haya mambo utajikuta huli..

Naamini mwili we binaadam ni A COMPLEX LABORATORY EVER.. Tumekaririshwa mbaya kwamba the unit Cell huzaa tissue, Na unit tissue huzaa organ Na unit organ huzaa system Na unit system huleta a living organizm.. Na wanakwambia a Cell is a unit Na wanakuwekea mapicha Na mazagazaga Yao, lakini wanabailojia Wa viungo wanashindwa bado kinijibu swali langu kwamba seli zinazounda organ ya sikio ndo hizo hizo zinaunga organ ya Macho au korodani ???????!!!

Ukimchunguza mpishi..- huli..! Lakini turudi at origin .. Kula fresh food DAIMA..
 
aiseeeeeee! kazi ipo!! mpaka mtu kufikia kifo chake, atakuwa ameona na kusikia mengi! period!
 
tatizo ni hiyo zaidi? au kwa wingi ? ni kwa kiasi gani haswa hadi kitu hicho kiwe umekila kwa wingi? huu wingi ndio shida kwangu au kila mtu ana wingi wake unaomdhuru.
wale wanaokula makande shule za bweni na ugali na maharage toka form 1 hadi 4 kila siku, hawa watakuwa hawali kwa wingi? na mbona wanadunda tu na afya njema kabisa.
kwa hiyo nafikiri hili neno wingi ninahitaji maelezo ya kina kumsaidia mtu kuelewa na kuepuka kula vitu fulanifulani. la tutakuwa tunageneralize mno.
 
madaktari wa tiba ya sayansi ya mzungu na tiba mbadala wanashauri sana kila mlo wako usikose kachumbari ambayo inakuwa na nyanya ndani yake tena mbichi ili kusaidia uyeyushaji wa chakula sasa zimekuwa sumu tena.
 
viazi na nyanya vina kiasi kidogo sana cha sumu (solanine na tomatine ) kuweza kumdhuru mlaji, vile vile baadhi ya viazi na nyanya hasa zina lycopene na beta carotene kwa wingi ambazo zinafanya kazi kinyume na hiyo sumu ya solanine.
 
 
Kama ni hivyo, sumu ni nzuri kwa afya zetu maana kila kitu tunachokula kina sumu na bado tunadunda tu! haya madhara ya kansa na nini ni ajali kazini.
 
Kwetu nyanya zinalimwa sana na bibi zangu wanatumia siku nyingi mpaka leo nina
bibi yangu anakaribia miaka mia na yuko fit.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…