Sikuzote kumuita msichana Demu huwa siwezi, na hili neno kulitamka kwenye kinywa changu ni zito sana kwakweli. Na kwa nilivyokuwa nikidhani hapo awali nilikuwa najua kama kunmuita msichana demu ni kama kumdhalilisha flani hivi. Ila naona linatumika sana kwakweli, lakini sijui kwa nini hili neno kwangu mimi linakuwa ni zito kulitumia. Sasa wadau na hasa kina dada wa humu JF naomba mnieleweshe vizuri kama hili neno mnakubaliana nalo kuitwa hivyo au huwa hampendi mnapoitwa mademu?
Definition of dame: lady - mistress - madam - gentlewoman
dem ni Ng'ombe jike...
Kaunga...Hili neno si la kiswahili. Ni neno ambalo limeanza kutumika dhidi ya akina dada miaka michache iliyopita sidhani kama imefika hata miaka 20 tangu lianze kutumika nchini. Ni neno ambalo asili yake ni Uingereza.Na maana ya kiswahili? I mean waswahili tunavyosema demu tunamaanisha nini?
nyie mnavyoitwa buzi mna ngozi kwani?
BAK si tumelikopa na kulipa maana yetu? Na limeonekana ni tatizo, ndio maana nataka kuelewa ili niseme kwamba it is okay kwa mimi kuitwa Demu au siyo!
Nakubali ni neno la kiingereza na maana zake kwa huko si mbaya hadi watu walichukie!