Hivi wakulima waliikosea nini nchi hii? Ni watu wanaoonekana hawana thamani hata kidogo!

Hivi wakulima waliikosea nini nchi hii? Ni watu wanaoonekana hawana thamani hata kidogo!

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Mkulima wa Tanzania ni mtu asie thaminiwa kabisa hata kidogo. Hii imefanya kuonekana kilimo hakika tija. Hata umshauri kijana akitoka SUA ajikite kwenye kilimo Bado hata kuelewa.

Hapa kitaa kuna jamaa yetu baada ya kutoka SUA Moja kwa Moja, alianza kujifunza kunyoa na baada ya kujua Leo hii ana saloon pamoja na kuwa Diploma ya kilimo. Awamu karibia zote mkulima amekuwa akitelekezwa sana bila ya msaada wowote.

Mkulima unalima Kwa mbinde sana huku ukiuziwa pembejeo feki za kilimo kama mbegu,madawa na hata mbolea muda mwingine inamfikia tiyari Isha expire!

Mbegu, dawa na mbolea unauziwa Kwa bei ya juu sana kiasi kwamba hata utunzaji wa mazao Yako unakuwa hafifu halafu bei unakuja kuuzia bei mbaya mbaya sana isiyokuwa na manufaa kwako mkulima na serkali hiyo hiyo iliyokuletetea pembejeo feki na za bei ya juu inahusika Moja Kwa Moja kukudidimiza chini badala ya kukuinua.

Hata vifungashio bado mkulima katelekezwa serkali haina habari naye na Wala haijari. Tumeshaomba tuwe tuna nunuliwa Kwa kilo lkn Serikali yetu haizingatii kabisa mkulima anaibwa Hadi yeye mwenyewe anajionea huruma pekee yake.

Gunia/roba la kg100 lkn Bado linafungwa lumbesa Hivi hii ni haki kweli?

Hiki kinachofanyika ni wizi wa waziwazi kabisa. Iko Hivi Mimi kipindi nauza nyanya zangu Hivi karibuni mnunuzi anakuja na kreti zake anajaza Hadi juu kabisa(nitaweka picha) baada ya hapo ikihesabika limejaa Hadi nyanya inadondoka linawekwa pembeni na linapungunzwa Hadi kuwa flat na zinazo punguzwa zinawekwa Kwa kreti jingine hizo ndo faida ya dalali hivyo akijaza kreti tatu tu Tyr linajaa na la kwakwe!

Kwenye mpunga napo Hali ni Ile Ile kipindi cha nyuma walikuwa wanatanua yale madumu ya kupimia mpunga/ mahindi.

Njia zilizokuwa zinatumika ni hizi.

Kwanza unatafutwa mchanga wenye ujazo wa Ndoo husika hasa Yale ya Rangi maarufu cora au madumu ya Mozambique (mozabiki) yanachemshiwa maji ama mafuta ya kupikia yanachemka kabisa then ule mchanga unaweka kwenye ndoo husika halafu mafuta au maji yanawekwa mle kwenye ndoo na inafunikwa Ili ilainike na kutanuka.

Iikilainika ule mchanga unakuwa unashindiliwa(kama anatwanga kwenye kinu) huku ukiongezwa mwingine Hadi mhusika aridhike kabisa kwamba limetanuka ipasavyo.

Sasa baada ya kugundulika kuwa wanafanya wizi huo ikabidi waje na njia ya kutingisha gunia/roba lile la mpunga au mahindi.
IMG-20240916-WA0003_1.jpg
Sasa hii njia wakawa hawapati faida kama mwanzo ikabidi wawe wanaenda kiwandani inakotengenezwa hii mifuko/ roba inatolewa oda ya mifuko hata 1000 yenye ujazo mkubwa.

MFANO: Mfuko unaweza kuwa na urefu sawa tu na mfuko wa debe6-7 lkn huu uliotolewa oda na maelekezo maalumu upana unakuwa ni mpana zaidi.

Hivyo akija Kwa mkulima kupima na akitingisha aisee kwenye gunia lako la debe sita kawaida litaishiamo na mengine utachota kama debe 2+ kulijazia la mnunuzi.

Huu wizi umefanyika sna Kwa wakulima wa mpunga mwaka huu.

Niombe Kwa wizara husika ya kilimo. Bila kupepesa macho waziri wa kilimo mh Hussein bashe .

Pembejeo zinazotolewa na serikali Bado bei Iko juu sana kiasi kwamba mkulima wa Hali ya chini hawezi kumudu gharama za manunuzi ya madawa,mbegu,na mbolea kwani bei inakuwa juu sana.

Imagine mfuko wa mbolea DAP kg50 unanunua 80-85 bei ya ruzuku hii. Halafu gunia la zaidi ya kg100 la vitunguu,mpunga na mahindi unauza 45-60k Wakati wa msimu wa mavuno huo ni wizi na hii ni Ni aibu kabisa Kwa serikali.
IMG-20240916-WA0004.jpg
Serikali itapata hasara Gani iwapo mfuko wa mbolea utauzwa japo 30-40k Kila aina ya mbolea?

Mbona Kodi inapanda Kila Leo lakn mazao mkulima mnamuacha soko ajitafutie mwenyew Kwa wahuni?

Hapo Kwa majirani wakenya mkulima anathamani sana na vijana wengi wanajiajiri kwenye kilimo na ufugaji na wanaofanikiwa sana.

Kenya Kila kitu kwao hawakumbani na vitu feki iwe mbegu, madawa na mbolea vyote watakuambia viko kwenye ubora.
IMG_20240623_183944_912.jpg
Huku ukija kwenye mifugo ndo usiseme kabisa chanjo haziaminiki kabisa unaweza chanja kuku wako baada ya wiki mbili ama tatu tu ugonjwa ukija unapuruni kuku wako wote unabaki kujiuliza si nimechanja hata mwezi Bado haujaisha huu?

Naomba kuwasilisha machache haya kati ya mengi kutoka Kwa wakulima.
IMG_20240623_183932_454.jpg
 
We piga pesa ndefu kama hutoheshimiwa
 
Hapo hapo hujazungumzia kipimo cha kg na uchakachuaji wa mizani, wanunuzi watu wabad
 
Nilishawahi kulima mihogo, wakati wa kuuza nikapata mteja kiroba Cha kilo 25 kikijaa nalipwa 20,000. Basi boss mnunuzi akatuma vijana wake kuja kuchimbua ila kuja kupanga/kupima ni yeye mwenyewe boss atakuja. Mihogo ikachimbwa kama robo heka hv akili ikashtuka nikawaambia acheni kwanza mwiteni boss wenu aje apime kwanza. Kaja boss kaanza kupanga kwenye kiroba aisee ule upimaji nilitamn kulia na ndio mwisho wa kujihusisha na kilimo ulianzia hapo
 
Nilishawahi kulima mihogo, wakati wa kuuza nikapata mteja kiroba Cha kilo 25 kikijaa nalipwa 20,000. Basi boss mnunuzi akatuma vijana wake kuja kuchimbua ila kuja kupanga/kupima ni yeye mwenyewe boss atakuja. Mihogo ikachimbwa kama robo heka hv akili ikashtuka nikawaambia acheni kwanza mwiteni boss wenu aje apime kwanza. Kaja boss kaanza kupanga kwenye kiroba aisee ule upimaji nilitamn kulia na ndio mwisho wa kujihusisha na kilimo ulianzia hapo
Kwakweli mkulima analiwa mno kwenye Nchi hii. Mnunuzi ndo anajipangia apime vipi na anunue Kwa bei ipi tunatatizo kubwa sana
 
Back
Top Bottom