Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
Walimu kama hawa ndiyo maana kwenye mahafali ya darasa la saba hawaibuki. Hawa ndiyo waliozifanya shule nyingi zianze na sherehe kabla ya kukabidhiwa vyeti.
Vinginevyo, ni vitasa kwenda mbele. Mtu unaanza la kwanza mpaka form six, umechapwa bakora za makalio zaidi ya mia tano. Makalio yanakuwa magumuuuu, hadi mwiba unadunda.
TIcha wa hivi washasakwa sana na manati kitaa, ila nao wanakuwa na machale sana, unaweza kumsaka mwaka mzima umuoni, siku ukimuona, hasira zimekwisha, amekuwa rafiki yako.