Hivi wamiliki wa vyuo vya vikubwa vya kati vya afya ni wanasiasa walioko madarakani?

Hivi wamiliki wa vyuo vya vikubwa vya kati vya afya ni wanasiasa walioko madarakani?

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Vyuo vya afya vinavyotoa diploma vimekuwa vingi sana kitu ambacho ni chema.

Lakini katika wingi huu,umeingia ushindani usio halali wala sawa katika kunyang'anyana wanafunzi.Kuna uhuni mkubwa baadhi ya vyuo vikubwa wanafanya lakini mamlaka zilizopo zinawachekea tu.

Mamlaka kama Nactvet kuwachekea watu wanaovunja sheria,taratibu na kanuni za uendeshaji wa vyuo hivi,ni dalili tu ama wanakula mlungula ama wanawaogopa wamiliki ambao katika hali ya kawaida hawawezi kuwa watu tu wa kawaida.

Kama ni kweli wanasiasa ndio wanamiliki baadhi ya vyuo vikubwa tu hapa nchini,basi kusema kweli hivi vyuo vinaharibu sana elimu na maisha ya watanzania kwa kuwa vimekuwa kama mazimwi ambayo hayaogopi sheria wala hayadhibitiwi.Vimekuwa kama magenge ya wauza madawa ya kulevya kwa jinsi walivyo na nguvu.
Nactevet wameshindwa kuwadhibiti na wanawabembeleza tu na kuwasaidia kufanya uovu.

Kuna watoto wengi hawajaingia kwenye mfumo kisa watu wachache wenye tamaa ya fedha waliowaiba kutoka vyuo vingine lakini hawawezi kuwasajili kwa kuwa mfumo unataka mwanafunzi afutwe alikosajiliwa kwanza.

Kama ni suala la mazingira ya rushwa yaliyotengenezwa kimfumo,naomba Takukuru waingilie kati kwa kuomba taarifa za wanafunzi walio nje ya mfumo na wawahoji vizuri watagundua uozo mkubwa sana kwenye hizi mamlaka.

Kuna mengi ya hovyo ikiwepo kuzidisha idadi ya wanafunzi wakati walimu ni wachache kwa uwiano unaotakiwa kisheria.

Hapa waziri unapaswa kuwachunguza hawa Nactvet na kufanya mabadiko makubwa ya uongozi ijapo hawa walipo wameshakuwa wabobevu kwenye mifumo.

Kama wamiliki ni wanasiasa badi tuombe Mungu tu siku wakijisikia kufuata sheria wafuate
 
Kwan unadhan kwann D nne, unaruhusiwa kusoma Diploma ya CO.

Hawa wahuni ndio wanaodidimiza Mfumo wa Elimu, unaozalisha vilaza wengi Kwa Imani ya "Kila kitu utakijua kazini".


Vyuo vyao bila D , visingepata wanafunzi.
 
Hivi adimins hamuoni kichwa cha habari kimekaa vibaya mkarekebisha?!!
Kwani Kazi yenu ni nini!!?
 
Back
Top Bottom