Masanja Mkandamizaji ametajirika kwa kilimoweng wao wametajirika mfn erick shigongo, james mwangamba
Ilo nalo nenofundi hujenga kwa wenzake kwake kuna vuja! hata hivyo makungwi wengi ndoa zao zimevunjika
Mkuu umeongea point sana aisee. Hili swali Mimi huwa najiuliza sana hili swali. Wanatupa njia ambazo wanadai ni za kufikia mafanikio wakati wao wenyewe hawana hayo mafanikioHivi hawa wanaotoa elimu ya ujasiriamali wanautajiri kiasi gani?
na hawa wanaosema kilimo kinalipa tena mpaka wanatoa gharama zake na faida wao nao wana utajiri kiasi gani toka waanze.
ASante
Mimi naomba nijikite hapo kwenye RED tu.Yawezekana ikawa kweli na yawezekana ikawa si kweli ...
Mosi, tanguliza Imani Moyoni ...
Pili: Weka maarifa kichwani
Tatu: Weka pesa Mfukoni.
Pesa ni hatua ya mwisho baada ya hatua mbili za awali, Ya kwanza ni ya muhimu sana - kama unaamini kwamba inawezekana - ITAWEZEKANA TU! Kama unaamini kwamba haiwezekani - HAITAWEKANA KAMWE.
BADALA YA KUKATISHANA TAMAA TUTIANE MOYO!
Binafsi naamini yale yanayoongelewa ni ya kweli kabisa! Kabla hujajaribu usiwakatishe wenzio tamaa.
Nafikiri kuna makundi mawili..kuna kundi linalofundisha ujasiriamali na kundi la pili wao ni watoa hamasa tu wanawaita motivational speaker. Kundi la pili ni ajili ya kukujengea uwezo wa kujiamini na haliitaji mtu kuwa mjasiriamali. Kwenye kundi la kwanza ni muhimu mtoa ushauri awe amewahi kufanya hicho kitu anachoshauri. Ni hatari sana kupokea ushauri kwa mtu ambaye hana uzoefu na biasharaMimi naomba nijikite hapo kwenye RED tu.
1. KUJARIBU: Siungi mkono majaribio yaliyobase kwenye illusions. Mimi ni shuhuda wa wamama wengi wanaoaminishwa kuwa jambo fulani linaweza kufanikiwa halafu baadaye linabakia kuwa majuto kwao.
Wakati MTAALAM MUELEKEZI anawaaminisha waelekezwa, yeye huchukua fedha yake ya ada na kusonga mbele, waelekezwa mara nyingi huishia kukutana na changamoto ambazo hawakuzitaraji. Mwisho wa siku wanaishia kuwa wadaiwa sugu wa FINCA na PRIDE kwa kufuata maneno ya mtaalam wa maneno.
2. KABLA HUJAJARIBU: Hapa naunga mkono phase B ambayo wewe hukuitaja. KABLA HUJAJARIBU USIWAAMINISHE WENZIO KUWA INAWEZEKANA.
Tutor B, si kila jaribio linafaa kwa afya. Ujasiriamali ni uwekezaji. Uwekezaji unahitaji study na sio inspiration peke yake. Mtu mmoja anawaambia wenzake UKUMBINI Diamond Jubilee juu ya ufugaji bora wa kuku, lakini hajui kuwa kwenye Agro-Vet Shops kuna madawa feki kwa kuwa yeye binafsi hafugi. Muelekezwa kwa kukosa kwake kulifahamu hilo, anaingia kwenye uwekezaji huu wa 'kusadikika' in full measure. Anachanja kuku lakini kuku bado wanakufa. AMEPOTEA kwa kumfuata muuza maneno ambaye hayaishi maneno yake.
Mimi siku zote nitawashauri wanaotaka kusonga mbele, ukitaka kujifunza kilimo, kajifunzie shambani. Hawa wanaokusanya watu kwenye halls kwa fedha ni wachumia tumbo.
Hakuna jambo lililowahi kuwezekana kwa kuwa tu mfanyaji anaamini linawezekana. Jambo huwezekana ikiwa tu vigezo vya kuwezekana kwake vimefikiwa.
mawazo finyu haya... fikiria kwanza mwalimu wako wa msingi, sekondari na chuo. (kama umesoma lakini) wako wapi sasa... mtu kuwa na elimu na kitu na kukitoa kwa watu haina maana umpekue na kujua kafanikiwa vipi kwanza... cha kushukuru yeye kawa muwazi kwako ili kama ni safari ya mafanikio muwe wote kama utamfuata ila kama utaona njia yake haikufai pita hivi.... nyie ndo wale wale msiotaka kuthubutu mnataka mlale maskini na kuamka tajiri..Hivi hawa wanaotoa elimu ya ujasiriamali wanautajiri kiasi gani?
na hawa wanaosema kilimo kinalipa tena mpaka wanatoa gharama zake na faida wao nao wana utajiri kiasi gani toka waanze.
ASante