Hivi, wanaume mnaposema kuwa wanawake wa siku hizi tunapenda usawa huwa mnamaanisha nini?

Best comment ever!

 
Makosa ya category ipi???
 
Ndiyo ila naona kama hii slogan wanaume huwa mnaimisquote sana ndo maana nikauliza ninyi wanaume kwa upande wenu mnaposema wanawake tunapenda haki sawa huwa mnamaanisha nini?
Tunamaanisha mnataka hadi mkojoe kwa kusimama[emoji23][emoji23][emoji23] au sisi tukojoe kwa kuchutama[emoji23][emoji23][emoji23] (joking)
 
Haupungukiwi kitu..

Ila jee mume ana tabia gani kwako?.mke huwezi jenga mwenyewe

Mfano tu
Yeye ni mwaminifu pia?mana km sio uchungu rohoni huo

Je yeye ana kauli nzuri kwako pia?...
Sample tu hio

Pande zote mbili wajitathmini..havielei .,vinaundwa
 
Hili dude lina misongo ya kufikisha muda mrefu bila olewa
Nakuona hakimu wa maisha ya watu hongera ila kama unahisi kuwa tunayoyaandika humu ndo yanayotutambulisha uhalisia wetu basi pole utapata taabu sana kuwaza maisha ya mtu usiyemjua kutokana tu na maneno yake ya nyuma ya baobonye
 
Hesabu ya ndoa ni 1+1 = 1. Ikiwa tofauti na hilo jibu ndo yanaanza hayo uliyouliza
Ndoa haina kanuni moja kama ambavyo Maisha hayana kanuni moja tusilazimishe wote kufuata kanuni moja bila kujua kwamba maisha au ndoa ni kama mtihani ambao kila mtu ana maswali yake tofauti na ya mwenzie na tunapofeli ni pale tunapotaka kuiga majibu ya wengine wakati kila mtu ana maswali yake
 
Umeelezea mengi ila je ni wanaume wangapi wanaokuwa na shukurani na wanaolipa fadhila kwa wake zao wanaofanya hivyo? Zaidi wanaume wengi shukurani yao na malipo yao ni kusaliti wake zao na kuzaa watoto nje ya ndoa kitu ambacho hata kwenye maandiko kimekatazwa

Halafu naomba nikurekebishe hapo kwa wazungu hivi unajua kuwa kwa wazungu hata kufanya kazi za nyumbani na kulea watoto linachukuliwa kama ni jukumu la wote mwanaume na mwanamke kama ambavyo kutafuta pesa na kuhudumia watoto linachukuliwa kuwa ni jukumu la wote?

Yaani kwa wazungu siyo ajabu baba kuamka asubuhi kuwaandalia chai familia yake na kuwakaribisha mezani huku mkewe amelala na wala haumwi pia kwa wazungu siyo ajabu baba kumbadilisha mwanaye pampers wakati mkewe yupo na hana kazi yoyote sasa jiulize wanaume wa kibongo mnaweza kufanya hayo?

Hamuwezi na kwa sababu hamuwezi na bado mnachukulia kwamba ni majukumu ya wanawake ndo maana hata sisi bado tunachukulia kwamba kutafuta pesa na kuhudumia familia ni majukumu ya wanaume na tukifanya tunafanya kwa kusaidia tu hivyo hapa msitulaumu bali ni kutokana na mgawanyo wa majukumu na kutokana na wanaume kukataa kuyabeba majukumu yetu kama ya kwenu ilihali mnataka sisi tuyabebe majukumu yenu kama ya kwetu
 
Yaani kumbe hivi hiyo dhana ya kwamba mwanamke ndo chanzo cha maovu yote duniani mnaichukulia serious? Mimi nilijua mnaisemaga kiutani kumbe mko serious kabisa? Yaani eti Evah kula tunda ndo kawa chanzo cha matatizo yote duniani na siyo shetani tena? Hebu kasome maandiko ni wapi paliandikwa hayo yote unayosema na uache kupotosha na kujitungia maneno yako mwenyewe ambayo hayapo

Kasome tena kitabu cha mwanzo na utagundua kuwa baada ya kula tunda ndipo mwanaume aliambiwa atakula kwa jasho lake na atamtawala mwanamke na kwa mujibu wa biblia hayo maneno aliyatamka Mungu mwenyewe lakini hakuna sehemu aliyosema kuwa mwanamke ndo chanzo cha dhambi zote duniani wala hakuna sehemu aliyosema kuwa mwanaume ilibidi awe mtawala tangu mwanzo narudia tena HAKUNA kama ipo niletee hilo andiko hapa sasa hivi

Hivyo hayo sisi hatuyajui na ndo mara ya kwanza nakusikia wewe unayatilia mkazo wakati hayapo sisi tunachojua ni kwamba kama mwanaume umeamua kufuata maandiko basi fuata maandiko yote ya kumtawala mwanamke na kula kwa jasho lako ukishindwa kufuata andiko la kula kwa jasho lako basi pia na andiko la kumtawala mwanamke usilifuate

Maana haiwezekani mchague maandiko ya kuyafuata na maandiko ya kuyaacha acha porojo zako hizo fuata maandiko ya kwenye biblia yaani hauna hata aibu unaongea kitu ambacho hakipo umekijaza kwenye ubongo wako mwenyewe ndo ukitumie kupotosha watu wengine?
 
Sidhani kama ni kweli, sjawahiktoka nje ya tz, ila ntafatilia kama ni kweli wanaume wa kimarekani wanawabadrishia nepi watoto
 
Hakuna aliyeniambia na ndo maana nikauliza ili mnipe jibu basi tusifanye mambo kuwa magumu nijibu hilo swali langu NDIO au HAPANA?
 
Mazingara ya kudhalilishwa mnayajenga wenyewe(baadhi yenu).
Kwa sababu gani na kwanini mtudharau na mtudhalilishe wanawake wote kwa sababu ya maovu ya baadhi ya wanawake?

Je na sisi tutakuwa sawa tukiwajumuisha wanaume wote kwa sababu ya maovu ya baadhi ya wanaume?
 
Haupungukiwi kitu..

Ila jee mume ana tabia gani kwako?.mke huwezi jenga mwenyewe

Mfano tu
Yeye ni mwaminifu pia?mana km sio uchungu rohoni huo

Je yeye ana kauli nzuri kwako pia?...
Sample tu hio

Pande zote mbili wajitathmini..havielei .,vinaundwa
Asante
 
Sidhani kama ni kweli, sjawahiktoka nje ya tz, ila ntafatilia kama ni kweli wanaume wa kimarekani wanawabadrishia nepi watoto
Kama wewe kitu haujawahi kukisikia wala kukishuhudia basi haimaanishi kwamba hakipo au hakijawahi kutokea na mimi naongea out of personal experience kwa sababu nimeshuhudia kuwa ni kweli wanafanya hayo tena imekuwa kama sheria kabisa

Kwa maana kwamba mume au mke ambaye hafanyi majukumu yoyote kati ya hayo anaweza kwenda kushitakiwa na mwenzake na sheria ikachukua mkondo wake tukiachana na haya tunayoyaona kwenye movies na series ila kiuhalisia pia ndiyo maisha yao halisi something which is fair kwa sababu kusaidiana na kuingiliana majukumu hakubadilishi jinsia ya mtu
 
Nnauhakika sijakosea kitu.

Baada ya kuumbwa vitu vyote ndipo aliumbwa mwanaume na akapewa mamlaka ya kuvitawala na kuvipa majina vyote.

Baadae akaumbwa mwanamke kama msaidizi wake, na mwanamke pia alipewa jina na mwanaume. Hapo ilikua ni kabla ya maswala ya kula tunda.

Na pia skusema mwanamke ndo chanzo cha maovu yote. Ila nlimanisha aliefanya interaction ya kwanza na shetani na kumconvice mwanaume kushiriki dhambi ni mwanamke(kitu ambacho kinafanyika kila siku), hapo ndo ulikua mwanzo wa kula kwa jasho na kuzaa kwa uchungu. Hapo ndipo mwanamke alishushwa cheo ktoka MSAIDIZI hadi MTAWALIWA.
 
Tangu nmeanza kuangalia movie sjawahi ona mwanaume ananepisha mtoto, au mwanaume anapika chakula cha nyumbani na wanawake wapo.


Labda ni kwasabab mara nyngi hua naangalia movie za kivita ;
 
Hivi wanaume mmeshakaa mkajiuliza ni kwanini Mungu aliwapa mamlaka ya kututawala ikiwa hamjatuumba wala hamjatuzaa? Hamjui kwamba hiyo mamlaka ilikuja na gharama zake za kutuhudumia na kutimiziwa wajibu wenu kwetu? Ndo maana nakwambia kwamba kama umeelewa vizuri maandiko basi utagundua kuwa mwanaume kumtawala mwanamke vinashabihiana na mwanaume kula kwa jasho lake

Sasa haiwezekani wewe mimi nijilishe nijivishe tena nikulishe nikuvishe halafu bado unataka unitawale hivi inakuja hiyo? Yaani kusaidiwa majukumu yenu mnataka ila kuchukuliwa nafasi zenu ndo hamtaki? Mkuu narudia tena mwanaume alipewa atawale vitu vyote kabla hajaumbiwa mwanamke ila alivyoumbiwa mwanamke hakupewa mamlaka ya kumtawala hadi pale walipokula tunda ndipo Mungu ilibidi aseme sasa kwamba mwanaume utamtawala mwanamke na pia utakula kwa jasho lako

Na pia mwanaume kumtawala mwanamke bado haikubadilisha nafasi ya mwanamke kuwa kama msaidizi kwa sababu Mungu ndicho alichokikusudia tangu anamuumba mwanamke na hakuna sehemu alipotengua kauli yake kuwa mwanamke siyo msaiadizi tena kumbuka hata makamu wa rais ni msaidizi wa rais lakini bado yuko chini ya rais na anatawaliwa na rais kwahiyo kuwa mtawala haimaanishi kwamna ndo siyo msaidizi hapana lakini sasa wewe unataka unitawale mimi hivi hivi tu wakati haujaniumba wala haujanizaa?

Hiyo nafasi mliyopewa hamkupewa bure bali mlipewa na gharama zake sasa wanaume wengi hiyo nafasi mnaitaka ila gharama zake hamzitaki kitu ambacho hakiwezekani na ndo maana ndoa nyingi ambazo mwanamke ndo mtafutaji mkubwa unakuta mwanamke ndo anatawala nyumba hiyo ni nature tu na hamuwezi kutulaumu hata siku moja makamu wa rais hatakiwi kufanya majukumu mengi kuliko rais na ikitokea hivyo huyo rais lazima tuwe na mashaka naye na lolote linaweza kutokea
 
Tangu nmeanza kuangalia movie sjawahi ona mwanaume ananepisha mtoto, au mwanaume anapika chakula cha nyumbani na wanawake wapo.


Labda ni kwasabab mara nyngi hua naangalia movie za kivita ;
Nilitaka nianze kukushangaa ila mwishoni ulivyosema hivyo nimeona siyo kosa lako hayo mambo yapo na tena kwa wazungu wameyaweka kama sheria kabisa ila wabongo sijui shida nini yaani sijui mnataka wanawake wanawake ndo wafanye majukumu mengi kuliko wanaume? Yaani kwa kifupi wanaume wa kibongo mnataka mteremko kwenye kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…