kwa ufupi nilichogundua since niingie JF (kulingana na mawazo ya wanaume walio wengi )ni wanaume wengi kutopenda mwanamke anayewa-possess too much. wengi utasikia hawapendi kuulizwa ulizwa uko wapi, unafanya nini, uko na nani, simu za kila dakika, na kero zingine za kuchungwa chungwa na kuonewa wivu. sijajua sababu ya wao kutopenda kuwa possessed ni coz wana ugube gube au nini ila hyo ndo observation yangu.
kwa mantiki hii mimi ninazo hizo tabia zote za kuwa too possessive. nikitaka nimpate wa kumatch nae ni lazima niwe kama kondoo yani mengine nijifanye tu mjinga na kufoji kuwa na vitu ambavyo kiukweli sina