Hivi wapo waliochomoka kimaisha kwa kutegemea mshahara wa chini ya million 1 tu?

Tatizo kuwapata hao watu waaminifu
 
Nikweli, manake kwa ukwasi huu hapana
 
Mimi binafsi kipato changu kwa mwezi hakizidi laki 7 lakini kwa sasa namiliki nyumba ya kisasa na mwisho wa mwaka huu naagiza gari kwa ajili ya usafirishaji..kila kitu ni mipango na malengo...jitathimin na jielewe kidogo kina maana kuliko kikubwa
Tupe siri ya mafanikio mkuu
 
Hata ungepewa mshahara 10mil bila kujiongeza kijasiliamali sio ufisadi!! Ujasiliamali na biashara huchomoki. Utaishia kununua nguo na kujenga nyumba na kubadilisha mboga tu.

Lakini ukiwa na mawazo ya kinasiliamali hyo 1mil ni mtaji mzuri tu kwani zipo fursa zinazoweza kuimeza hyo au 2mil na ukapata faida nzuri
 
JIBU ndio. Uthibitisho, rejea watumishi wa umma kama Mtemi Endrew chenge, Nazir karamagi, Edward Lowassa, engineer Fredrick Sumaye, Dr kafumu, AG Wereme, AG mwanyika. Hawa wote wameishi kama watumishi wa umma na mawe waliyonayo hakuna wakuwagusa.
Wanalipwa below 1m?
 
Ndio, na wametusua balaa, ishu ni kupanga budget vzur mkuu.
Wako wanaozidi hata 2M, but they live miserably.
 
hata mm nalipwa 280,000/= lakini nina pikipiki mbili :-Q :-Q :-Q :-Q :-Q :-Q :-Q :-Q :-Q
 
Acheni kujidanganya hao waosema wataacha Nazi ndio wa kwanza kuripoti kazini. Acheni kazi ili wanatafuta kazi wapate kazi, watumishi yoyote mwambie acha kazi kana ataacha jua kua anatoka familia tajiri kwanza kapewa gari (16 mil) kuendea kazini, pili kafunguliwa biashara (30 mil) kisha anajiita mjasirimali.

Hao wanawapa moyo tu. Mtoto wa mkulima usiache kazi Ndugu yangu wala usisikilize mawazo ya walionazo. Kama wewe unategemea jiwekee akiba kidogo kidogo kisha soma mazingira kwanza usikurupuke, pili usikope fedha yeyote kwa sasa watu wanalia Bodi ya mikopo inakwangua unabaki na fedha ya kuishi tu sasa ukikopa tu utaona cha mtema kuni. Hadithi za vyuoni ziache kwa utijipa matumaini kufanikiwa kwa muda mfupi kama miaka miwili, mitatu hali halisi sivyo.

Ukiona MTU kafanikiw kwa haraka achana nae kuna matatui

1. Ni fisadi
2. Anatumia nguvu za Giza.
3. Ni mwizi au anadhulumu watu.

Jiulize wazazi wako na wale waliokutangulia hawakuwa na akili ya kufanikiwa haraka haraka kama wewe. Baadhi ya wazazi wamejenga nyumba baada ya kusitaafu, je asinge walipia ada? je mngekuwa hapo sasa? Sipendi kuvunja moyo MTU ila tuambiane ukweli wanalisoma master na kusema nikimaliza master najiajiri wapi?

Ndio wa kwanza kuripoti kazini. Chukulia mfano wabunge wanapata kiasi ngani baada ya miaka 5? Kwa nini asiende kuazisha biashara au ndio wangangania kuakaa zaidi ya miaka 20 kwa nini? Kama fedha ya kutosha anayokuazisha biashara.

Kama mbunge anangangania je wewe je unayelipwa chini ya milioni eti nikiazisha biashara naacha kazi, huwa sipendi kauli ya kundangaya watu, tuambiane ukweli. Ukweli ni mchungu Lakini huna budi kuupokea. Tu kweli ni huu mishahara yetu ni ya kukidhi mahitaji yetu tu (chakula, ugonjwa, mavazi) si ya maendeleo.

Ukitaka kujenga au kuoa utaona ni shida kweli. Ujenzi wa nyumba ya familia utalazimisha familia kula maharage kila siku ili kusevu LA sivyo utaishia kupanga tu. Ukishajenga nyumba na kuoa, majukumu ya watoto yanakuja automatically mh...hapo ni bangumu zaidi kwani utataka mwanao spate elimu bora shida ni fedha???

Ukisha fanya hayo anza biashara kidogo kidogo kwa akiba niliyokuambia uweke hapo mwanzo. Hapo tegemea mafanikio baada ya miaka kumi tena bila mtoto wa pili, shehere na misiba. Pia lazima ujue biashara si mchezo au maneno ni kitu hatari, baadhi ya makampuni yanauza mabasi yao, wanapunguza wafanyakazi mfano Acacia wakati wao wanachimba dhahabu, kwanini waibe kwenye makinikia??

Ni shida. Hivyo Ndugu yangu kwenye biashara kuna vitu vitatu lazima upambane navyo
1. Kodi, makampuni makubwa yanakwepa kodi.
2. Rushwa au Takirima.
3. Wizi na mwisho
4. Dumba. Hili la mwisho ni shida.

Biashara nyingi wanatumia Ndumba(Juju). USHAURI: Kwa watu wa mjini Biashara ya M-PESA, Airtelmoney na Tigopesa inalipa kwa kiasi. Kwa watu wa kijijini, mazao kama Mahindi na Maharage yanalipa ila lazima ukubali madalali kwani ndio wanajua soko likoje. Hiyo ni machache tu.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…