Katika hili Warioba hausiki kabisa. Yeye alifuata ualiko aliopewa kwa kuwa yeye siyo mjumbe wa bunge hilo. Yeye alialikwa na Mwenyekiti awasilishe rasimu ya pili. Kimsingi haikuwa kazi ya Warioba kumdai mwenyekiti afuate kanuni kwa kuwa kanuni hizo siyo yeye aliyeziweka na kama kuna kubadili kanuni yoyote ni jukumu la wabunge hao wa bunge la katiba na Mwenyekiti wake. Kwa hiyo kilichotokea anayepaswa kulaumiwa ni yule aliyemwalika Warioba awasilishe rasimu ya katiba leo. Tungemshangaa sana kama asingetokea bungeni tayari kuwasilisha rasimu kama ambavyo alitakiwa na viongozi wa bunge hilo. Kwa kutokea na kutoendelea tumeweza kuelewa kuwa Mwenyekiti alisigina kanuni. Huo ndio ukweli. Mzee Warioba amekutana na zahama za wajumbe hao kuvutana tu kwa mujibu wa kanuni. Samwel Sita alipaswa kutafsiri kanuni kama zilivyo. Na ni kweli alionywa mapema kufuata kanuni akajifanya kichwa ngumu.