Hivi wasanii huwa hawana wivu kwenye mapenzi?

Hivi wasanii huwa hawana wivu kwenye mapenzi?

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
70,916
Reaction score
141,437
Huwa najikuta tu nawaza, mtaani kina da Mwaju wakijua wameshea au kuibiana mwanaume watazichapa si kitoto, ngumi za kuchana shumizi na gagulo dera litageuka kimono. Mara chache kwa wanaume kumaindiana kisa mwanamke japo inatokeaga pia.

Cha kushangaza kwa wasanii huwa ni tofauti utakuta wameshea, wamechukuliana ila zinaiva tu na kuitana dada, brother hivi hawana wivu?

Wema, Wolper, Jokate na Penny hawa ni wapenzi wa zamani wa Simba ila wanaiva tu bila shida.

Lulu na Wema ni marafiki zinaiva na walishawahi kuwa wapenzi wa Kanumba.

Wolper na Hamisa hawa walishakua wapenzi wa Diamond ila wako poa kabisa.

Majizzo na Diamond ni waume wenza kwa Hamisa wote wamezaa nae ila wako poa na wanasapotiana kazi zao.

Idris na Diamond ni waume wenza kwa Wema na wako sawa tu.

Aunt Ezekiel na Mwengi hawa ni wazazi wenzie Moze Iyobo na wako poa wanapostiana picha zao. Na wengine wengi.

Nawaza tu!
 
Madam vp ushamaliza likizo??[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ....
 
Wadangaji hao hawana mapenzi ya kweli na wakiume wanatafuta umaarufu wanakuwa na wanawake zao wengine kabisa sababu unakuta wana Chelewa kuoa wengi wao fatilia
Ukitaka kujua mapenzi ya kweli Ray na chuchu hansi ushawahi muona chuchu kampost johari [emoji53]
 
Kwa wanawake ukiona hawaoneani wivu ujue hawakupenda kweli au wanaidanganya jamii tuu lakini moyoni huwa wanaumia lakini muda ukipita wanakubali matokeo na kuanza upya urafiki..... Kwa wanawake huwa ni urafiki wa mashaka tuuu na kuigiza
 
Wadangaji hao hawana mapenzi ya kweli na wakiume wanatafuta umaarufu wanakuwa na wanawake zao wengine kabisa sababu unakuta wana Chelewa kuoa wengi wao fatilia
Ukitaka kujua mapenzi ya kweli Ray na chuchu hansi ushawahi muona chuchu kampost johari [emoji53]
Kumbe, Wema alishawahi sema mwanaume aliempenda kuliko ni kanumba ila still hakua na wivu na Lulu wana mioyo mizuri
 
mbona na ww kwenye dp yako umeva chupi ? mume wako haoni wivu kama utadongonewa na wengine?
 
Mie hata jamaa nliemuacha enzi za vita vya maji maji nkimuona leo yupo na friend angu nita.....
hahaaa ..hao ni mapaka ..mitoto ya mjini maslahi mbele..mapenzi baadae "" hawawezi kugombania papuchi au dushe bila uwepo wa maslahi'' never
 
Kuna party zinatokea wanajikuta 10 wamemshea mmoja nayy yumo humohumo,,,dooo. Mi siwezi
 
Back
Top Bottom