Hivi wasanii wa Tanzania mlizaliwa kuwa wasanii tu

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Habari za ijumaa wakuu na wadau wa jukwaa hili wasalam

Kuna hii tabia ya baadhi ya wasanii wa Tanzania hasa wa zamani kung'ang'ania kurudi kwenye game wakati mda wao umeshapita.

Kila kitu na wakati wake wakati wao umeshapita wakubali tu na haiwezi kuwa Kama zamani hata wa kirudi kwenye game kwani zama zimebadilika Sana wakubali matokeo.

Hawa ni baadhi ya wasanii wanaolazimisha au media kulazimisha wawe juu ila wakati umewatupa mkono ,

1.saida karoli 2.q chief 3.matonya 4.ray c 5 mb dog 6.chidi benzi 7.dully Sykes 8.keisha 9.z anto

Wapo wengi ila hao ni baadhi yao wakubali matokeo na wapambane na Hali zao Kama walishindwa kuwekeza kipindi hicho ndo imekula kwao.
 
 
Waliozaliwa na Vipaji ni wachache, wengi ugumu wa Maisha ndo umepelekea kuwa na Vipaji sasa unafikiri wataishije???
 
Wajifunze kutoka kwa msanii Inspector haaroun...!

Yeye ameyakubali matokeo mapema kabisa, na kwa sasa anajishughulisha/amejikita katika biashara, anapambana kujiongezea kipato kuendana na hali pamoja na kasi ndani ya Tanzania ya Viwanda..!

Ila wasanii wamuelewe, ikiwa atajitokeza wa kuimba Mashahiri hasi (ya hovyo) hawezi kuwafumbia Mdomo, ataingia Studio na kuwajibu/kuwarekebisha katika kuwarudisha katika KWELI...!
 
Unapata shida gani wakirudi hata kama ni wazee? Haki yako iliyovunjwa ni ipi?
 
Kuna kufanya mziki biashara na mziki kipaji. Kama wanafanya kipaji ni sawa Ila Kama wanafanya biashara nadhani wapumzike
 
Au ndiyo msemo wa “Don’t hate the game, hate the player don’t be mad”.
 
Kama bado wanatoa burudani hakuna tatizo.sauti zisizo na mpangilio ndo kelele tu.mbona kina Don William wamezeekea kwenye game
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…