Hivi wasanii wanalipa kodi

Mapensho star

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
3,052
Reaction score
4,104
Nasikia kila siku wasanii wanapiga shoo ndio kipato wanachotegemea sana
sasa nachojiuliza sijawahi kusikia kama hili jambo linaongelewa sana kuhusu wasanii wa bongo fleva kulipa kodi mana naona tra kama wamewakomalia wafanyabiashara tu mtu unakabiashara tu kadogo hakaeleweki inabidi ulipe kodi sasa nataka kujua ni diamond tu ndio anaelipa kodi au ni wasanii wote mana sijawahi kusikia
Je tra huwa wanasimama milangoni kipindi mashabiki wanaingia kweny show? au wasanii wanalipia kodi zao moja kwa moja basata?
na wasanii naona wanasema wanapiga show moja mil 1 hadi mil 5 na wanafanya video za mil 20 hii imekaaje
 
NADHANI WANA VITAMBULISHO VYA MJASILIAMALI VILE VYA ELFU 20 KWA MWAKA.
 
wasanii wengi wa bongo hawalipi kodi kwani bongo muziki ni biashara isiyo rasmi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…