Hivi wasanii wanalipwa pesa na media

Hivi wasanii wanalipwa pesa na media

Davion Delmonte Jr.

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2013
Posts
2,149
Reaction score
1,718
Nilisikia huu utaratibu kwamba watakuwa wanalipwa pindi nyimbo zikipigwa redioni. Hivi ni pesa ngap? Inafika elfu hamsini kwa siku ? Ama kuna utaratibu gani unatumika?

Mi naona hamna realistic kabisa kama itakuwa ni pesa mbuzi. Maana hata nyimbo nyingi zinazopigwa ni za wasanii wakubwa waliotoka tayari sasa mfano ndo umpe elfu 50 ama hiyo pesa ambayo naamini itakuwa ndogo itawasaidia nini? Bora wangeachana na hii kitu

Na hata kama ni kulipwa hakuwezi kuwa na scale moja ya kulipa maana nyimbo ya msanii kama Diamond inavuta attention ya watu wengi hivo huwezi fananisha na nyimbo ya wasanii wengine wadogo wadogo. Kwa hiyo sidhani kama wasanii watalipwa kwa kiwango sawa.

kwanza ingepaswa msaanii mkubwa kama Diamond asisambaze nyimbo zake kwenye radio bure, radio wanapaswa wanunue tena kwa bei kubwa sana. Imagine Diamond anatambulisha ngoma mpya radioni Je ni watu wangapi watataka kuisikia? watu kibao na hivo basi nyimbo ya Diamond inavutia matangazo kwa radio ambayo yanakuwa na tozo kubwa na faida kubwa kwa radio. Mameneja wa D fanyia kazi hili suala. Ameshakuwa msanii mkubwa hamna haja ya kusambaza nyimbo bure tena radioni
 
Elfu 50 kwa siku ni hela ndogo?...Ungepewa nafasi ya kupendekeza..ungetaka walipwe shilingi ngapi?..Btw bado hawajaanza kulipwa
 
Wengine wakiwa wanatumbua majipu nyie ndo kwanza mnayazalisha
 
Kuna mada kuhusu hii ishu humu. Hayo yote yalijadiliwa, itafute ujue namna na makadirio ya ulipwaji wa mirahaba kwa wasanii. Aidha hii issue tulisema mapema haiwezi kufanikiwa kuna watu walibisha sana ila sasa wanajionea haijaanza na wasanii wenyewe ndio wameanza kuipinga
 
Mi mshangao wangu kwa kiongozi huyo alietoa hili wazo inamaana hakufikiria uwezekano na mikakati ya kulifanikisha hili?
 
Mi mshangao wangu kwa kiongozi huyo alietoa hili wazo inamaana hakufikiria uwezekano na mikakati ya kulifanikisha hili?
Walikurupuka si Kidogo. Huu mfumo ni mgumu sana kufanikiwa hasa kwa nchi za Africa (refer Kenya). Mfumo wa digital Bado haujakomaa enough hata kujua wimbo umepigwa mara ngapi kwa siku kwenye vituo mbalimbali. Njia za ukusanyaji, ulipaji wa hiyo mirahaba hazijakaa sawa. Kifupi kuna loopholes kibao si ajabu wasanii wenyewe ndio wanaongoza kupinga huu mfumo sasa
 
Na hii ndio aina ya viongozi tulionao. Hawafikirii in and out ya jambo kabla ya kuliamu na kutangaza wao ni kukurupuka tu.
 
Elfu 50 kwa siku ni hela ndogo?...Ungepewa nafasi ya kupendekeza..ungetaka walipwe shilingi ngapi?..Btw bado hawajaanza kulipwa
Hiyo hela kwa wasanii kama Diamond ni ndogo sana aisee. Ila kwa wasanii wadogo itawatoa sema shida ni kwamba kwa wasanii wadogo uwezekano wa nyimbo kipigwa radioni ni mdogo sana.
 
Back
Top Bottom