Hivi wasomi wa serikali akiwemo Kailima walisoma vyuo gani?!

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,734
Reaction score
140,476
Katika kujenga hoja yangu naomba nitoe mfano mdogo. Juzi Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi akitoa tamko la kuifuta Chadema katika uchaguzi. Tume hiyo inaongozwa na wanasheria na wataalamu mbalimbali.

Mbali na maelezo ya Dkt. Nshala ambaye ni Chadema, ukisikiliza mawakili mbalimbali waliohojiwa katika media inaelezwa kwamba kuifuta Chadema kwenye uchaguzi ni kinyume na sheria. Mawakili hao wameongea kisheria wakinukuu kanuni zilezile alizotumia Kailima.

Sio hayo tu, mawakili wa serikali wamekuwa wanashindwa kesi nyingi mahakamani. Wasomi wa serikali wamekuwa wakifanya maamuzi ya hovyo sana kiasi cha kuitia serikali kwenye hasara kubwa.

Unajiuliza hawa wenzetu walisoma vyuo gani? Walitumia vitabu hivi hivi vya vyuoni au kuna vitabu vingine vinavyofundisha ujinga?
 
Human herding in politics is an occurrence of entrusted people suspending their individual reasoning because of flattering or working towards group objectives and hypocrite

Unyumbu wa kisiasa ni tabia ya wanaopewa dhamamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki), kwasasa uchawa tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo, a.k.a kujizima data

Hata mimi nilifikiri kama wewe baadae niliamua, (kuzama kwa undani) kufuatilia kwa kina kuhusu wasomi nikaja na hiyo dhana ya kimombo na kwakiswahili ninadhana zaidi ya 5, (concepts)
 

OKW BOBAN SUNZU ficha ujinga wako hata kidogo basi.​

 
Kwenye hiyo Tume hakuna Wataalamu wa maana, wamejaa maafisa vipenyo na jaji wa mchongo
 

Shida ya wataalamu wakiingia serikalini, wanafanya maamuzi yao ili kuwafurahisha wateule wanasiasa, kutaka wapendwe na wengine kama hao kina Mkurugenzi, ndio maana unaona amerudishwa pale wakati wa uchaguzi kwani anajulikana atafanya nini, hawezi kusimamia usomi wake hata kama anajua anachofanya sio sawa na atatetea. Atafanya kila kitu kwa kufurahisha walio mteua wanasiasa.
 
Alisomea sheria Havard we umesomea nini na wapi. Toa kwanza boriti kwenye jicho lako.
 
Kairima alisoma shule ya msingi NGURUKA.... KULE UVINZA
 
We na nyumbu wenzio km huyo Nshalla ni husda na wivu, uwezo wenu ni mdogo hamuwezi kuonekana. Hizo nafasi ni kwa watu waliotulia wenye uwezo mkubwa kiakili. Angalia wenzio kina David Silinde, Patrobas Katambi wamewaacha humo mmebaki na stress wenzenu wako mbali kimaisha.
 
Wamesoma vyuo vile vile ila wanatumia akili za ccm kufanya kazi zao
 
Hao ni wasomi wajinga
 
Tatizo nchi hii siasa inaongoza utaalamu,,nchi nyingine hasa zilizoendelea hawako hivyo.
 
Watafuta vyama vyote vya upinzani sasa, maana tutahamia chama kingine cha upinzani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…