Hakuna umri maalumu wa kuanza kujua haya masuala kwa watoto. Ni mara tu akili yake inapopevuka. Wanasayansi wanasema akili ya mtoto ni kalin sana kushika vitu. Vinaweza vikawa vyema au vibaya pia. Unaweza kupima tu kwa kunagalia jinsi anavyozingatia yale unayomwambia hata ukimdangaya (kwa mfano ukimweleza neno kuwa ni "matusi" nae akashika hivyo hivyo mpaka pale atakapojua si "matusi"tena kupitia mtu mwingine.
Chanzo cha kujua jema na baya kwa watoto pengine ni mazingira anayokulia na kulelewa. Yaweza kuwa alisikia na anajifunza kutoka kwenu wazazi wake, wakubwa zake kiumri katika familia ikiwemo wale wanaomlea kila siku, watoto wenzake anaocheza nao hapo nyumbani, mtaani au huko shuleni, vipindi vya kwenye TV nk.
Nakumbuka siku moja nilikuwa nyumbani kwa Mzee wangu Mdogo, tukiwa sebuleni na mwanae wa kike (sasa amekuwa) wakati huo alikuwa na miaka 4. Katika ITV, kuna muziki ukapigwa wa Kimagharibi jamaa alionekana akimkumbatia na kumbusu mwanamke, kabinti kale kadogo wakati huo kakaangalia pembeni na kuzuia macho yake kwa viganja vya mikono kakasema hakawezi tena kuangalia TV kwa kuwa watu wanabusiana na kukubatiana..kwa kweli hata mzee mwenyewe alizima TV , akaguna tu na kushindwa kuuliza mtoto kajuaje haya kuwa ni mabaya!.
Watoto inabidi kuwafuatilia kila hatua ya makuzi yao na pengine kujaribu kupeleleza wanapokuwa wakicheza na wenzao kujua hata lugha wanazotumia...unaweza kudhani mwanao hajui kitu kumbe ndio gwiji la kufundisha wenzake mambo yasiyofaaa huko mtaani na kama una lala nae chumba kimoja akawa anaanika kila kitu unachokifanya na mzazi mwenzio kwa wenzake.