Hivi wazazi mnajua hatari kiasi Gani inawakabili watoto WADOGO mnaowaachia smartphones muda wote?

Hivi wazazi mnajua hatari kiasi Gani inawakabili watoto WADOGO mnaowaachia smartphones muda wote?

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

I declare interest, Mimi Rabbon ni baba wa watoto wengi, mtoto yeyote popote ni mwanangu sababu Mimi ni mwalimu wa watoto kiimani na kiroho.

Twende haraka kwenye mada, zipo athari nyingi wazazi mnawaletea watoto wenu Kwa kujua na wengine kutojua.

Ninakutana na cases mbalimbali, mtoto mwenye umri wa miaka chini ya minne anavaa miwani ya macho👀, na shida hiyo ya macho wengi Si ya kurithi, HAPANA ni smartphones!!

Siku hizi familia nyingi Zina uwezo wa kumiliki smartphones, sasa wazazi wengi Kwa uvivu, hutaki mtoto akusumbue, unanunua data Kisha unamwachia simu aperuzi kuangalia cartoons nk nk

Sasa wengine hata usimamizi wa karibu hamna, limit ya muda hamna, mtoto utamkuta chumbani taa zimezimwa anaangalia cartoon, hamjui kuwa kuangalia simu gizani kunaua haraka sana macho na uwezo wa kuona?

Mtoto chini ya miaka mitano, smartphone ya nini kumwachia? Leo mzazi una miaka 20-30 macho mazima, unaona sawa mtoto wako miaka chini ya 5 aanze kuvaa miwani? Akifikisha miaka 30 Si atakuwa kipofu?

USHAURI:

1. Mtoto chini ya miaka mitano usimpe smartphone, mwekee vipindi maalum vyenye mafunzo kwenye tv aangalie Kwa muda maalum Kwa usimamizi wako, na hakikisha Kuna mwanga wa kutosha sebuleni.

2. Acha mara Moja kumzoeza mtoto chini ya miaka mitatu kumpa smartphone, umri huo Si sahihi Kwa mtoto kuangalia simu Kwa ukaribu sababu Yeye hajui kuregulate mwanga.

3. Hakikisha mtoto wako anahudhuria mafunzo katika nyumba za Ibada Ili apate chakula Cha Roho pia.

4. Msomee BIBLIA au hadithi za BIBLIA Kutoka kwenye smartphone au vitabu ulivyonunua Ili kumsaidia kupata Elimu na Maarifa ya Mungu Ili kukusaidia malezi Bora. Pata muda wa kujielimisha Ili uweze kuwa msaada Kwa mwanao.

HITIMISHO:

Mungu amekuamini na kukupa watoto Ili uwalee, unatakiwa umlee mtoto wako katika njia impasayo maana hatoiacha hata atakapokuwa mtu mzima akiwa na macho yote yanaona!!

Mungu awabariki.

Karibuni🙏
 
We buana ni kitu gani utatumia hakina madhara? Hivi kuna kitu chenye balaa kama PAPUCHI? nani ameiacha kwa 7bu ina madhara? Pamoja na neno yoote lakini kuna wajomba wanabugia kama andazi sasa hivi habari sijui nini peleka kuleee
 
We buana ni kitu gani utatumia hakina madhara? Hivi kuna kitu chenye balaa kama PAPUCHI? nani ameiacha kwa 7bu ina madhara? Pamoja na neno yoote lakini kuna wajomba wanabugia kama andazi sasa hivi habari sijui nini peleka kuleee
Mabatchelor mnaharibu Uzi.

Oeni na mpate watoto ndipo mjue kuchangia vizuri.
 
Wanalilia Chim ya dadii tunapungza mwanga tunampa tu

CC😛alina
Mtoto akianza kuangalia video U-Tube Kwa smartphone akiwa na miaka miwili, miaka mitano anavaa miwani,

Akifikisha miaka 18 ni kipofu!!
 
Kuna kitot miaka 3 kinatumia smartphone vibaya mno aisee ,nilikapa nikaone lol eti kawasha data fasta, kaanza na youtube, kaja tiktok, kulikuwa hamna game kaingia playstore karuka ruka adi kakutana na game nikaona huyu hapana nikampokonya asije danload mchele bure
 
Kuna kitot miaka 3 kinatumia smartphone vibaya mno aisee ,nilikapa nikaone lol eti kawasha data fasta, kaanza na youtube, kaja tiktok,kulikuwa hamna game kaingia playstore karuka ruka adi kakutana na game nikaona huyu hapana nikampokonya asije danload mchele bure
Mbali na kuangalia video za porno,

Smartphone zinaua sana macho ya watoto,

Wazazi tuache uvivu, mtoto anahitaji usimamizi wa karibu, TV inatosha tena Kwa vipindi maalum na muda special.
 
Back
Top Bottom