screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,857
- 15,866
Huyu jamaa licha ya watu kusema ana gundu ila mimi naona sio gundu tu, ni kwamba menejimenti yake pia haimpush vile inavyopaswa. Nimeshuhudia mara nyingi Mbosso/Zuchu na boss mwenyewe wakiandaliwa zinduzi mbalimbali za Album/EP kwa gharama kubwa, huku wakipewa promo kubwa na Wasafi Tv/Redio bila kusahau machawa wao lakini sikumbuki kama Lavalava amewahi kufanyiwa hivi. Hata ukikakaa kwenye TV yao nyimbo za Boss, Mbosso na Zuchu zinachezwa sana kuanzia mpya hadi za zamani, lakini ni nadra kuona nyimbo za Lavalava. Na si kwamba Lavalava hatoi ngoma kali, ana nyimbo nzuri nyingi tu. Je, wana mpango gani na huyu mtu pale WCB mbona anaishi kama mtoto yatima?