Hivi weupe ndio urembo au?

Mtu wa namna hiyo hana tofauti na anayejichubua sababu nae hataki afahamike kama ni mweusi. Ni yale yale ya kukataa ngozi, nywele, majina kifupi utumwa wa fikra

Na huo ndo ujinga [ignorance] wenyewe sasa!
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] Toooooba!
 
Mkuu umenena vyema kabisa!
 
Wewe hujawahi kusikia ila zipo. Na mashiko yangu mimi wewe unaweza kuona ni upuuzi...ndo hivyo tunatofautiana

Naam, na ndivyo hivyo hivyo kwenye kujichubua na kushonea nywele bandia.

Wewe unaweza usione mashiko ya sababu za mtu kujichubua ilhali yeye anaona akijichubua ndo atakuwa mzuri zaidi.
 

 
Wewe unataka uzungu unaficha Sanga unabaki na Josephine Goodluck Paul mwingine anajichubua. Wote lengo ni moja- Uzungu ila njia tofauti.
Hahaa sawa mkuu kumbe mtu unaweza kujikataa asili yako kwa namna nyingi
 
Waafrika ni wahanga na watumwa wa mapokeo ya tamaduni na mila za kigeni, tangu tulipoaminishwa kuwa za kwetu ni za kishenzi na ki mizimu na ukweli tumekuwa watumwa mpaka tunagombana wenyewe kwa wenyewe, kugombea imani za kigeni inakera.

Ukiangalia mabara mengine yamebaki na tamaduni na mila zao achilia mbali majina yao pia. Shida iko Africa. Ukija kwa wake zetu na binti zetu wao ndiyo kabisaa wameukana asili yao eg rangi, nywele. Huwezi kuona mambo haya mabara mengine sisi tumepokea kila kitu. Mpaka utu wetu umekosa maana mbele ya jamii nyingine
 
Sio urembo wala nini ni ULIMBUKENI tu, wanaojichubua kutoka weusi kwenda weupe wengi wao HAWAJIAMINI
 
Wanaume wa dar naona siku hizi wanajichubua sijui ndo iweje sasa au sijui kuna faida yoyote
 
wakati mweusi alikua very beautiful and young, since ajibadilishe amekua ugly and old. lol.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…