yupo hivi.. ananywele nyingi lkn zenye afya murua kama mti ulao mbolea!,si mwembamba wala mnene,mweupe kiasi anapua ya size macho mekundu kiasi huku yakipendezeshwa na nyusi nyeusi zaidi ya mkaa,mrefu,mwenye kifua kipana.. mwili wake kiujumla unaonyesha ni mtu anaetumikia kifungo cha mazoezi enye mikono nadhifu iliyoshiba misuli! huku akipendezeshwa na miguu mikakamavu yenye manyoa kama kichwa chake kilivyohubiri hapo kabla.. tembea ya kikamavu mithili ya simba ateteae mahali pake,mwenye jicho makini kila aendapo..mbali na hayo yote sura yake bado inahubiri amani furaha na uchangamfu ikiwa kama kificho cha weledi wa uchunguzi makini ndani yake!.