Hivi ya BALALI yameishia wapi??

Mzee wa Gumzo

Senior Member
Joined
Apr 21, 2008
Posts
197
Reaction score
5
Kila uchwao maswali mengi hujipanga kichwani mwangu mzee wa gumzo lakini huwa sipati majibu.

Jamani naomba tusaidiane hili la balali,si mnamkumbuka yule gavana wa benki kuu ya tanzania aliyepewa nafasi hiyo akitokea (kuazimwa)IFM?.

Baada ya kuibuka kwa sakata la EPA na rais kumvua ugavana tulitarajia kuona kasi,hari na nguvu mpya katika kumkamata balali na kumfikisha mbele ya pilato kama shahidi wa kwanza na muhimu katika uporaji wa mabilioni ya wadanganyika.

Lakini mpaka leo kimyaaaa!.Hatusikii chochote kuhusu mtu huyu.tuliambiwa alikuwa marekani anatibiwa lakini mpaka leo?

Hivi kwa ishu nyeti kama hii mpaka leo balali anavinjari tu mitaani?Tunahitaji nini kumkamata? au tunaogopa nini?au niseme watawala wetu wangwaya nini kumleta balali mbele ya mkono wa sheria???

Mimi wala sielewi,labda nyiye wadanganyika wenzangu mnajua zaidi yangu!haki ya nani hii nchi!
Uwanja wenu waungwana
 
Hivi nani anatakiwa kutupatia jibu?
 
 
hata wabunge hawakutaka kujua alipo huyo mzee wa shoka sembuse siye pangupakavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…